Tuesday 17 June 2014

MWANAMKE:JE UNATAFUTA MCHUMBA? FUATA KANUNI HII,HAKIKA UTAMPATA MCHUMBA MWENYE TABIA UZITAKAZO

Kuna kitu kinaitwa nguvu ya mvuto, lakini
pia huenda mmeshawahi kusikia au
kusoma kitabu kinachoitwa "The Secret." Ni
kitabu kizuri sana kinachoeleza kwa kirefu
na kwa lugha nyepesi inayoeleweka jinsi
nguvu hii ya mvuto inavyofanya kazi. Katika
kitabu cha The Secret mwandishi Rhonda
Byrne anasema kwamba mawazo yetu ni

kama sumaku. Kwa kawaida sisi wanadamu
tumezungukwa na nguvu ambazo
hatuzioni lakini zipo kwa hiyo Kwa jinsi
tunavyofikiri hayo mawazo yanakuwa na
nguvu ambazo zinavuta kila kitu
tunachowaza, kiwe kizuri au kibaya, ni
lazima kitarudi kilipotoka, ambapo
sipengine bali kwako wewe mwenyewe.
Rhonda anazidi kubainisha utendaji wa
mawazo yetu kwa kutoa mfano wa ufanyaji
kazi wa Luninga (TV). Kama wote
tunavyofahamu kuwa ili kituo cha kurusha
matangazo ya Luninga kifanye kazi
kunakuwa na minara inayosafirisha
mawimbi na kuyageuza katika mfumo wa
picha na hivyo kutuwezesha kuona
matangazo ya luninga tukiwa majumbani
kwetu. Wengi wetu hatufahamu mitambo
hiyo inafanya kazi namna gani, lakini
tunafahamu kwamba kila chaneli ina
mawimbi yake ambapo kila tukichagua
chaneli fulani tunapata picha katika
luninga
zetu. Tunachagua mawimbi kwa
kubadilisha chaneli na ndipo tunapopata
picha za matangazo kutoka katika chaneli
hiyo. Kama tunataka kuona picha na
matangazo tofauti katika luninga zetu
tunabadilisha chaneli kwa kutafuta
mawimbi ya chaneli nyingine.
Sisi kama wanaadamu tuko sawa na mnara
wa kurusha matangazo ya luninga na tuna
nguvu kuliko minara ya kurusha matangazo
iliyowahi kuwepo hapa duniani. Mawimbi
yetu ndiyo yanayoratibu maisha yetu na
ndiyo yanayoifanya dunia iwe kama livyo
leo, kwani tunatengeneza mawimbi
kutokana na namna tunavyowaza. Ile picha
tunayopata au tunayoiona kupitia mawazo
yetu, sio sawa na ile tunayoiona katika
luninga zetu sebuleni kwetu, bali ni picha ya
maisha yetu! Mawazo yetu yanatengeneza
mawimbi na yanavuta kila tunachokiwaza
na kuwa ndio maisha yetu halisi.
Iwapo tunataka kubadili chochote katika
maisha yetu, basi inatulazimu tubadili
chaneli na mawimbi kwa kubadili namna
yetu ya kufikiri. Mwandishi huyo
anaendelea kusema, kinachosabisha watu
wengi wasipate kile wanachokitaka
maishani ni kwa sababu wanafikiria zaidi
kuhusu kile wasichokitaka badala ya kile
wanachokitaka. Hebu tujaribu kuchunguza
mawazo yetu na kauli zetu, tutagundua siri
kubwa. Kwani nguvu ya mawazo ipo na
inafanya kazi. Ugonjwa mkubwa sana
unaowakabili wanadamu hapa duniani
karne kwa karne ni ugonjwa
wa "sitaki" au "sipendi," anabainisha mama
huyo. "Watu wameendelea kuacha ugonjwa
huu uendelee kutawala katika mawazo yao,
vitendo vyao na kauli zao, wakiendelea
kuzingatia yale wasiyoyataka au
wasiyoyapenda." Anamalizia kusema
mwandishi huyo.
Ugonjwa huo ndio unaowatesa baadhi ya
wanawake wanaotafuta wapenzi. Mfano
halisi ni kauli kama, "mimi sipendi
wanaume wafupi," au "mimi sipendi
kuolewa na mwanaume mnyanyasaji…." na
kauli nyingine zinazofanana na hizo. Ukweli
ni kwamba kitakacho watokea
wanawake
wenye kutoa kauli kama hizo ni kuishia
kuolewa na wanaume wa aina hiyo…..
kinachofanyiwa kazi na mawazo yetu ya
kina (Unconscious Mind) ni kile
tunachokitamka, iwe ndicho tunachokitaka
au tusichokitaka, mawazo yetu ya kina
hayajui neno sipendi au sitaki, hukuletea
kile ulichokitamka na kukijaza katika akili
yako.
Kuna wanawake wengi ambao wameolewa
au wamewahi kujenga mahusiano na
wanaume ambao waliwahi kutamka
hadharani kwamba kamwe hawatoweza
kujenga mahusiano nao au kuolewa nao.
Hayo ni matokeo ya kauli zao ambazo
walizitamka bila kujua madhara yake. Kwa
hiyo basi kwa kutumia kanuni hiyo ya
mvuto kama alivyosema mwandishi Rhonda
Byrne mnatakiwa kuanza kuratibu mawazo
yenu na kauli zenu kwa kutamka aina ya
wanaume ambao mngependa kujenga
mahusiano nao au kuolewa nao na haiishii
hapo ni vyema mkajiweka katika mazingira
ambayo yatawavuta kuelekea mahali
ambapo mtakutana na aina ya wapenzi
muwatakao. Huwezi tu kukaa nyumbani
kwako au kutembelea eneo moja hilo hilo
kila siku halafu utarajie kukutana na aina ya
mpenzi umtakaye itakuwa ngumu, labda
uwe na bahati sana.