Saturday 21 June 2014

FAHAMU MUDA SAHIHI WA KUFANYA TENDO LA NDOA

Somo hili linaweza kukushangaza msomaji
wangu, kutokana na ukweli kwamba
ufanyaji mapenzi, hauwezi kuupangia
muda, lakini katika hali ya kawaida ipo
tofauti kubwa ya kufanya mapenzi, mchana,
usiku, alfajiri na nyakati za joto na kelele
nyingi za wapita njia.

Utofauti huu ndiyo unaweza kutofautisha
hali ya kufurahia tendo kati ya mtu na mtu.
Hakuna ubishi kwamba watu wanaofanya
mapenzi nyakati za joto, hupoteza
msisimko wa tendo si tu kwa sababu ya
kuchoka haraka bali hata kwa kukinai
harufu ya jasho liwatokalo mwilini.
Sababu hiyo na nyingine nyingi, zitokanazo
na kutojua muda sahihi wa kufanya tendo
la ndoa, zimewafanya wapenzi wengi
kushindwa kuridhika au kupata raha stahili
wakati wa kujamiiana na wapenzi wao,
jambo ambalo linanipa sababu ya
kufundisha muda sahihi wa kufanya
mapenzi ni upi?
Kwa mujibu wa uchunguzi wangu, ambao
pia ulitiwa nguvu na
machapisho ya hivi
karibuni yaliyotolewa kwenye magazeti ya
The Sun, Mirrow na The Express ilibainika
kuwa muda muafaka wa wapenzi kufanya
tendo la ndoa na kufurahia ni kati ya 9:30
na saa 4:30 usiku, Muda ambao zaidi ya
wanawake 3,000 waliowahi kuhojiwa
kwenye utafiti ulioripotiwa na mtandao
mmoja hivi karibuni walikiri kuwa ufanyaji
tendo la ndoa huwa na msisimko zaidi.
Hata hivyo, muda huo ulikubaliwa na wengi
si tu kwa sababu una utulivu wa hali na
mazingira, lakini pia ni wakati ambao hisia
za mapenzi huamka kwa watu ambao
pengine walikuwa na majukumu ya kazi
mchana kutwa. Ukichunguza utabaini kuwa
wanandoa wengi nyakati hizi huwa
faragha na hata mafumanizi mengi hutokea
kati ya saa 3 na saa 4 usiku.
Utafiti wa kitaalamu uliochapishwa na New
Study hivi karibuni ulitoa tofauti za mawazo
ya kimapenzi kwa mwanaume na
mwanamke, ambapo ukichukua takwimu
hizo utabaini kuwa kilele cha mawazo hayo
lazima kifikie muda huo nilioutaja na kwa
sababu nilizozieleza hapo juu.
Inaelezwa kwamba mwanaume hufikiria
tendo la ndoa mara 13 kwa siku takribani
mara 5,000 kwa mwaka tofauti na
mwanamke ambaye anatajwa kufikiri mara
5 kwa siku na 1,825 kwa mwaka, mawazo
ambao yote yamebainika kutekelezwa zaidi
nyakati za usiku kwa muda huo niliotaja.
Hata hivyo wataalamu wengi walishindwa
kukubaliana kwa pamoja juu ya umuhimu
wa muda, lakini waliafikiana kupitia
ushahidi wa utafiti wa watu waliobainika
kufanya tendo la ndoa nyakati za saa 3 -4
usiku kiasi cha kuupa sifa muda huo kuwa
unafaa zaidi kufanya mapenzi na kupata
matokeo mazuri.
Ifahamike kuwa kinachozungumzwa katika
makala haya si uwezo wa
kufanya tendo la
ndoa, bali ni matokeo sahihi. Watu wengi
wanaweza kulima, kufanya kazi, kufanya
biashara, kucheza na hata kusoma nyakati
za joto, baridi sana na hata usiku na
wakapata matokea, lakini kitalaam
litakuwepo swali wamepata matokeo
mazuri, wamefurahi sawa na wale
waliochagua muda sahihi?
Huu ndiyo ujumbe wangu kwa leo, ni vema
wapenzi wakafanya uchunguzi na
kufahamu ni muda gani mzuri kwa
mazingira ya kwao kufanya tendo la ndoa,
vinginevyo wanaweza kufanya lakini
wakajikuta wanakinai mapema au
wakapata raha kidogo.