Saturday 21 June 2014

KWA NINI WATU WENGI HUOTA WANAFANYA MAPENZI

Miongoni wa makundi ya vijana hasa
wenye umri wa kati miaka 15-23 wengi
wao huota wakifanya mapenzi ndotoni,
lakini mbali na hao kuna watu wazima pia
ambao hukumbwa na tukio hili. Uotaji wa
ndoto hii umekuwa ukitafsiriwa na wengi
kwa maana tofauti tofauti, huku wengine
wakiuhusisha na ufanyaji mapenzi na

Majini.
Uchunguzi unaonyesha kuwa uotaji ndoto
za kimapenzi huwatokea hata watu ambao
hawajawahi kufanya kitendo hicho kabisa,
huku watu wanaofanya nao wakiwa ni
wale wanaowafahamu kwa sura au
wasiowafahamu. Wengi wamekuwa
wakijiuliza maswali mengi juu ya nini
kinachangia uotaji huu wa ndoto za
kimapenzi?
Kitaalamu ndoto hizi hutokana na mawazo
ya mtu husika ambayo yanaweza
kugawanywa katika sehemu mbili ambazo
ni MAWAZO YALIYO WAZI au YALIYOJIFICHA.
Mtaalamu wa masuala ya ndoto Daktari
Gillian Holloway anaeleza kuwa ndoto hizi
hufumbua maamuzi na hisia zilizojificha
nyuma ya ubongo.
Pamoja na tendo hili kuwa baya katika
mitazamo ya wengi hasa
kiimani, lakini
bado si kitaalamu halina ubaya kwa
kiwango hicho kwani mara nyingine
husaidia kutafsiri yale ambayo wahusika
hawakupata kuyafahamu kabla. Kwa mfano
vijana ambao hawajafanya mapenzi hupata
kutambua raha itokanayo na kitendo hicho
na hivyo kuwaamshia hisia za kimapenzi
ambazo pengine hawakuwa nazo hapo
awali.
Wachunguzi wa masuala ya ndoto
wanasema ndoto hizi zikitumika vizuri
zinaweza kusaidia kumpata mchumba
anayegusa hisia za moyo, aina ya mapenzi
yanayokufurahisha, haiba ya mpenzi
umpendaye na wakati mwingine huchangia
kuongeza uzalishaji wa homoni na
kupunguza msongo wa mawazo sawa na
mtu aliyefanya mapenzi laivu.
Hata hivyo watu wanaotajwa kutokewa na
kitendo hicho mara kwa mara ni wenye
tabia ya kuogopa wanaume/wanawake na
hivyo kuzikandamiza hisia zao, pamoja na
wale wanaochochea hamasa za kingono na
kutokuzikata, (mfano kufanya romance na
kuachana bila kuingiliana), wanaotazama
picha za ngono, wanaozungumzia sana
mambo ya kimapenzi na wale wanaowaza
sana wapenzi wao walio mbali.
Kwa maana hiyo ili mtu asiweze kutokewa
na ndoto hizo hana budi
kujizuia na
mambo hayo yanayotokana na uamshaji na
ukandamizaji wa hisia za kingono. Hii ina
maana ya utashi wa mtu wa kutopenda
kuota, lakini si kwamantiki kuwa uotaji huu
unauhusiano na mambo ya kishirikina au
kichawi kama ambavyo watu wengine
wanavyoaminishwa.
Mwisho kama kuna wanaodhani kuwa
ndoto hizi zimewadhuru kwa namna moja
au nyingine, wafahamu kuwa
kilichowadhuru si kuota ndoto hizo bali ni
wasiwasi wao unaotokana na kusikia na
wala si madhara kwa maana ya kuota
kwenyewe, kwani ikiwa ni ndoto hata
wanyama kama Mbwa, Paka na Sungura
nao huota wakifanya mapenzi, ushahidi
ambao unatosha kutupilia mbali hoja ya
ndoto kutokana na majini.