Wednesday 18 June 2014

JE? WAJUA KWAMBA, KUA NA HIPS AU MAKALIO MAKUBWA....NI ISHARA YA AFYAKITAALAM

Uchunguzi uliofanywa nchini Uingereza umeendelea kulipandisha chati
umbo la kibantu, kwa kusema kwamba, kuwa na unene zaidi eneo la
mapajani, katika makalio na katika mahips ni vizuri kiafya, na humzuia
mtu asipate matatizo yakiafya.Wataalamu wanasema kuwa, mafuta
yanayopatikana katika mahips, huondoa fati asidi mbaya kiafya ambazo

huwa na mada za kuzuia uvimbe ambazo huifanya mishipa ya damu isizibe.
Timu hiyo ya wachunguzi imesema kuwa, makaliao makubwa ni bora kuliko
mafuta ya zaida yanayojilundika
katika mzunguko wa kiuno, ambayo
hayasaidii chochote.Wachunguzi hao wamesema katika Jarida la Kimataifa
la Obesiti kwamba, sayansi inapaswa kuangalia jinsi ya kuongeza mafuta
katika eneo la mahips na pengine katika siku zijazo madaktari
watatakiwa kuangalia njia za kuyahamisha mafuta mwilini na kuyapalekea
katika sehemu za mahips ili kulinda afya za watu kutokana namagonjwa 
ya mishipa ya moyo na magonjwa mengineyo kama kisukari. Watafiti hao
wameeleza kwamba,kuwa na mafuta kidogo katika hips kunaweza kupelekea
matatizo makubwa ya umetaboli.Wataalamu hao wameendelea kusema kwamba,
ushahidi unaonyesha kwamba, mafuta yanayozunguka mapaja na sehemu za
nyuma ni vigumu kuyeyuka kuliko yale yaliyo katika kiuno.Ingawa suala
hilo linaonekama kana kama ni kinyume, lakini ni kweli kwamba
kutoyeyuka huko kuna faida kwani, wakati mafuta yanapoyeyuka kwa
urahisi hutoa mada inayoitwa cytokines ambayo huleta uvimbe katika
mwili.Mada za cytokines zinahusiana moja kwa moja na magonjwa ya moyo
na kisukari.Kuyeyuka
taratibu kwa mafuta katika mapaja pia husababisha
homoni ya adiponectin izalishwe kwa wingi na husaidia kudhibiti sukari
katika damu na jinsi mafuta yanavyochomeka.Dakta Konstantinos
Manolopoulos aliyeongoza utafitihuo kutoka chuo kikuu cha Oxford
amesema kuwa, la muhimu ni umbo na wapi mafuta yanakusanyika, na
kwamba unene wa mahips na mapaja ni mzuri kuliko unene wa
tumbo.ILAIKUMBUKWE MAKALIO NA HIPSI ZINAZOONGELEWA HAPO JUU NI
ORIGINAL TU..KWA WALE WALIO YAPATA DUKANI HAPA HAMHUSIKI.