Thursday 26 June 2014

Dalili za mwanamke anayetoka nje ya ndoa

Dalili za mwanamke anayetoka nje ya
ndoa hazitofautiani sana na zile za
mwanaume. Kuna maelezo ya kitaalamu
kwamba, mwanamke anapotoka nje ya
ndoa yake, inakuwa rahisi sana
kubainika au kufumaniwa kuliko ilivyo
kwa mwanaume. Hii inatokana na ukweli
kwamba, hisia zinakuwa na nafasi
kubwa sana kwa mwanamke, kwani
mwanamke huishi kwa hisia zaidi kuliko
mwanaume. Bado nasisitiza kwamba,
haipaswi na siyo sahihi mtu kuchukulia

dalili hizi kama ushahidi wa mpenzi
wake kutoka nje ya ndoa. Uchunguzi
kufuatia dalili ni muhimu sana.
Zifuatazo hapa chini ni baadhi ya dalili
zinazoweza kuonyeshwa na mwanamke
ambaye anatoka nje ya ndoa yake:
1. Kuchelewa: Kuna wakati mwanamke
anaweza kuaga kwamba anakwenda
saluni au kusuka, badala ya kurejea
kwa muda ambao umezoeleka,
anachukua muda mrefu hata mara
tatu zaidi. kuna wakati kwenda
sokoni huchukua saa kadhaa bila
kujali soko liko umbali gani. Kama ni
mara moja sawa, lakini ikishakuwa
zaidi ya mara moja huenda kuna
tatizo la kukosa uaminifu.
2. Kubadili maeneo: Hebu chukulia
kwamba, mwanamke amezoea
kwenda soko fulani la karibu,
hospitali fulani ya karibu, saluni fulani
ya karibu na hata nyumba fulani ya
ibada ya karibu. Unapoona anahama
maeneo ya karibu ya huduma na
kwenda ya mbali, bila sababu ya
msingi, huna budi kuanza kutuhumu
mwenendo mbaya. Siyo lazima
kuhama kokote kuwe na mwenendo
mbaya, lakini kama kuhama
kwenyewe kunatia shaka kwa sababu
maelezo ya kuhama huko hayana
msingi, mwanaume ana kila sababu
ya kuchunguza kama hakuna usaliti
unaofanywa.
3. Ununuzi usio wa kawaida: Kama
mwanamke anatoka nje ya ndoa yake
kwa ajili ya kupata fedha, basi
atakuwa na mabadiliko makubwa
katika mtindo wake wa manunuzi.
Atakuwa ananunua vitu vya thamani
kubwa kuliko uwezo wake,
atakuwa
na fedha nyingi tofauti na ambazo
angekuwa nazo na pengine kumiliki
mali kama nyumba kwa siri.
4. Kuzungumzia kuachwa: Kuna wakati
mwanamke anaweza kuwa anatoa
kauli za kuonesha kwamba, kama
mwanaume anaona vipi , wanaweza
kuachana. Kama kila penye ugomvi
kidogo tu mwanamke anakimbilia
kusema, "kama ni kuachana,
tuachane tu" hiyo inaweza kuwa ni
dalili mbaya kwa mwanamke
anayetoka nje ya ndoa kwa sababu
hana tena upendo na mumewe.
Lakini pale ambapo mwanaume ni
mkorofi, kauli kama hizi zinaweza
kutolewa, hata kama mwanamke
hatoki nje ya ndoa yake. Kwa hiyo
kabla ya kumtuhumu, mwanaume
anatakiwa awe mkweli kwa nafsi
yake kuhusu anavyomtendea mkewe.
5. Kusitisha uaminifu: Mwanamke
anayetoka nje ya ndoa, mara nyingi
husimamisha kumwamini mumewe,
yaani hayuko tayari kushiriki masuala
ya siri, ambayo wanandoa huwa
wanashiriki. Husita kumshirikisha
mumewe kwenye mambo yake
mengi. Lakini pia husita kumuomba
mumewe ushauri, kama alivyokuwa
akifanya siku za nyuma.
6. Kuacha kuvaa pete: Kuna sababu
nyingi ni kwa nini mwanamke
anaweza kuacha kuvaa pete yake ya
ndoa. Moja ya sababu hizo ni
kusalitiwa na mumewe au ndoa yake
kuwa kwenye misukosuko mikubwa
sana. Lakini nje ya misukosuko
mikubwa ya ndoa,
sababu nyingine
inayoweza kumpelekea mwanamke
kuvua mara kwa mara au moja kwa
moja pete yake ya ndoa, ni kuwa na
uhusiano nje ya ndoa yake.
7. Kuonesha wasiwasi: Kama
mwanamke anatoka nje ya ndoa
yake , ni lazima atakuwa na wasiwasi
na mashaka yasiyo na sababu mbele
ya mume wake. Anaweza kuonesha
kutotulia kwa aina fulani kama
kwamba, anahofia kuna siri nitatoka
au kuna kitu ambacho tayari mume
wake anakijua dhidi yake. Mara nyingi
wasiwasi na mashaka humtawala
sana mwanamke anayetoka nje , hasa
katika hatua zake za awali za kutoka
nje.
8. Kuanzisha vurugu: Kuna wakati
mwanamke anayetoka nje ya ndoa
huanzisha vurugu za makusudi na
mumewe. Lengo la kuanzisha vurugu
hizo ni ili apate nafasi ya kujifanya
amezira na kuondoka nyumbani kwa
muda. Huo muda anapoondoka
nyumbani kujifanya kakerwa na
vurugu hizo ndiyo muda ambao
anautumia kwenda kwa hawara yake