Sunday 22 June 2014

Baadhi ya Wadada ni Mizigo Katika Mahusiano ya Kimapenzi

Leo itanibidi niseme tu hata mkinitusi
manake mmezidi jamani kuwapa mizigo
hawa kaka zetu alafu na wengi wao hata
hawashtuki mpaka pale mambo
yanapomwendea mrama, utakuta dada
mzuri kweli wa sura na umbo yupo kwenye
mahusiano na mkaka yaani huyo dada yeye

kazi yake ni kumchuna tu jamaa mara sina
vocha na hata ukimpa yeye kazi yake
kukubeep apigiwe mara leo sijui nimeona
nguo mwenge na mengine mengi ila
unakuta hakuna yeye kitu anafanya kwa
huyo mwanaume ili ajione
na yeye ni mtu
kweli , basi hata mawazo ya jinsi ya kupata
hela mpe basi , kazi yako wewe starehe tu
ijumaa ikifika ndo wakwanza kupanga
viwanja vya kwenda kujirusha hata hujui
jamaa yako hela kapata wapi...Alafu ndo
unakaa unajiuliza mbona siolewi? Bibie
Kuelewa yahitaji kujitoa usione Vinaelea jua
vimeubwa...