Monday 23 June 2014

Hisia zake utekwa ni kitu muhimu sana na wala si pesa zako we mfanyie hivi tu kama hatokuganda kama ruba.


1. KUWA NA MUDA NA MWENZI WAKO
Msingi wa kuwa na muda na mwenzi wako ni upamoja (togetherness) pamoja na kuwa kimawazo, kimwili na kiakili (focused attention). Kuwa na muda na mwenzi wako hatumaanishi kukaa pamoja kwenye sofa au makochi kuangalia TV; au movie hapo mnaipa time au muda wa
pamoja TV au movie mnayoitazama siyo mwenzi wako.

Kuwa na muda na mwenzi wako ni kukaa pamoja na kumpa attention yote, anaongea na wewe unamsikiliza tena ninyi wawili tu, kutembea pamoja yaani mmeamua kwenda kutembea kwa ajili ya kwenda kutembea wewe na yeye tu si kwa sababu mnaenda kanisani au mnaenda kazini, kupeana muda wa pamoja ni kama vile kwenda kula pamoja (outing) ninyi wawili na mkifika hapo kwenye hoteli mnaongea kwa kuangaliana ninyi romantically.


2. KUPEANA ZAWADI.
Zawadi ni kitu chochote unachoweza kukishika kwa mikono na kinakupa hisia kwamba aliyenipa zawadi alikuwa ananifikiria na ananipenda.Kutoa zawadi kulikuwepo miaka mingi iliyopita na tunazidi kurithisha kizazi hadi kizazi na kila mmoja naamini ameshapokea zawadi nyingi ingawa tunatofautiana katika upokeaji huo wa zawadi kwani kuna wengine leo inawezekana hawajapata zawadi, wengine hii wiki, wengine huu mwezi na wapo pia ambao huu mwaka bado hawajapata zawadi yoyote. Zawadi huelezea upendo, ndiyo maana hata katika uchumba kila upande hujitahidi kutafuta zawadi nzuri kwa ajili ya mpenzi wake.


3. MANENO MATAMU (Kusifia, kutia moyo na kushukuru)
Je ni mara ngapi umesema Asante au kumsifia spouse wako kwa jinsi alivyokurusha vizuri kwenye mahaba na sita kwa sita? Na je kawaida unapomsifia au ku-appreciate vitu anafanya huwa anajisikiaje?

Maneno mazuri au yanayotia moyo au yanayomsifia ambayo ni matamu husababisha mambo yafuatayo kwa mwenzi wako
(a) Huleta upamoja na ukaribu zaidi (intimacy)
(b) Huleta uponyaji kwenye majeraha ya hisia zake kama kuna maumivu moyoni mwake (healing) na kumfariji
(c) Mume wako au mke wako hujisikia kulindwa zaidi na anajisikia yupo katika mikono salama.

Jizoeshe kumsifia mpenzi wako kwa kila jema analolifanya ama kwa uzuri alokuwa nao, au kwa chakula kizuri unachopika au kazi anavyofanya au jinsi anavyowajibika mkiwa chumbani. Hapa wanaume tunahitaji kujitahidi zawadi naamini kutokana na mfumo wetu dume wa Kiafrika hata kusema asante au nisamehe au nimekosa inakuwa kazi, please naomba tubadilike.

5. KUSAIDIANA KAZI AU HUDUMA
Hii ni kufanya vitu ambavyo mwenzi wako anatarajia au anategemea ungefanya kuonesha unampenda na kumjali na kuwa wewe ni yeye ni kitu kimoja.

Inawezekana anategemea ungemsaidia kutandika kitanda, kusafisha nyumba, kupika, kufua nguo, , kuosha gari, nk hiyo mnaweza kufanya pamoja na ni njia nzuri ya kueleza kwamba unampenda kwa vitendo.

kama una nyongeza embu tupia comment yako au maoni yako kuhusu hili. I WILL APRECIATE IT.