Thursday 28 September 2017

TUNAOMBA RADHI KWA WADAU WA APP HII

SAMAHANI WADAU TUNAFANYA MAREKEBISHO KIDOGO YA APP YETU TUTARUDI HEWANI JUMAMOSI 30/09/2017

TUKIWA NA SIMULIZI MBALIMBALI MATUKIO NA VIDEO ZA YANAYOJIRI DUNIANI STAY WITH US

Tuesday 26 September 2017

Dk Mwakyembe akanusha kuifuta Miss Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ametolea ufafanuzi kauli yake na kusema kuwa hajasitisha mashindano ya Miss Tanzania na tuzo za muziki nchini bali ametoa angalizo kwa waandaaji wa mashindano hayo kuwa na uhakika wa kuyaendesha.

Cheche ya Ommy Dimpoz haikamatiki YouTube


Angalau kwa sasa Ommy Dimpoz anaweza akapumzika baada ya kuutua mzigo mzito wa lawama kutoka kwa mashabiki wake kuhusu kuchelewa kutoka kwa video ya wimbo wake mpya ‘Cheche’.

Picha: Pharell Williams aungana na mastaa wengine kupiga magoti

Mwanamuziki Pharell Williams ameungana na mastaa kama J.Cole, Steve Wonder na wachezaji wa timu ya (NFL)National Football Leagu kwa kupiga magoti ikiwa kama ishara ya kulaani tukio la mauaji liliotokea mwezi Agosti maeneo ya Charlottesville nchini Marekani.


Tazama picha mpya za Kylie Jenner baada ya kudaiwa ni mjamzito

Baada ya tetesi kuibuka hivi karibuni Kylie Jenner kuwa na ujauzito wa rapper Travis Scott, hatimaye mrembo huyo ameibuka kwa style mpya ambayo imeweza kuwashtua mashabiki.


Mrembo huyo ambaye anatoka katika familia maarufu duniani ya Kardashian, amepost picha mbili mpya kwenye mtandao wa Instagram ambazo zinaonyesha mrembo huyo kuna kila dalili kuwa hana ujauzito.

Video: Diamond na Zari wamekomesha ‘choko choko’


Siku ya Jumamosi ilikuwa ni siku ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Zari mzazi mwenzake na Diamond Platnumz.


Shughuli hiyo ilifanyika nchini Afrika Kusini, huku habari zikizagaa kuwa Diamond hawezi kwenda kuungana na mrembo wake huyo baada ya hivi karibuni kukiri kuchepuka na mwanamitindo Hamisa Mobeto na kuzaa naye mtoto wa kiume [Dylan].

VIDEO: Daktari wa Manji Utotoni Afunguka Mahakamani

Leo Septemba 25, katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam, ambapo mahakama hiyo imeanza kuisikiliza kesi ya Siku tatu mfuliulizo ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili mfanyabiashara Yusuf Manji mbele ya hakimu mkazi Cyprian Mkeha.

Picha: Kim Kardashian wa India awatoa mate vidume

Duniani wawili wawili kama sio jina basi mfanano wa sura au mwili, huko nchini India kuna dada anaitwa Sarah ila maarufu kama Kim Kardashian hii ni kutokana na umbo lake kuwa lenye mvuto kama mke wa rapper Kanye West.


Rais Magufuli amaliza ziara kwa kupiga marufuku

Rais Dkt. John Magufuli amemaliza ziara yake katika Mkoa wa Arusha hii leo huku akisisitiza kwamba ni marufuku kwa mfanyakazi yeyote kuhamishwa katika kituo chake cha kazi pasipo kulipwa stahiki zake.

Joti atoa shavu kwa vijana

Kama unakipaji kwa nini ufe na njaa, haya ni baadhi ya maneno yanayopatikana katika ngoma ya ‘Mtazamo’ iliyofanywa na Profesa Jay, Afande Sele na Solo Thang.


Kudhihirisha maneno hayo mchekeshaji nguli Tanzania, kutoka Orijino Komedi Joti ambaye kwa sasa anafanya kazi zake binafsi za uchekeshaji ametoa shavu kwa vijana waliyo na kipaji cha kufanya sanaa ya uchekeshaji ambayo anafanya.

Amber Lulu awachana wasanii wenzake (+video)

Wimbi la video vixen kuhamia katika kuimba limeonekana kukuwa kila kukicha. Amber Lulu amewachana wasanii ambao wamekuwa wakiwachukia warembo hao wa video wanapoamua kuingia katika tasnia ya kuimba.

Fedha zanunua Penati za Neymar kwa Cavani PSG

Mmiliki wa klabu ya Paris Saint-Germain bilionea Nasser Al-Khelaifa ameonyesha jeuri ya fedha kwa kumtangazia mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay, Edinson Cavani ofa ya Euro milioni moja aridhie kumwachia Neymar Jr jukumu la upigaji penati ndani ya klabu hiyo.


Neymar Jr [kushoto], bilionea Nasser Al-Khelaifa [katikati] na Cavani [kulia]

Wiz Khalifa amemruhusu 21 Savage kuwa baba mlezi?

Ule usemi wa ukipenda boga penda na ua lake, upo mpaka mbele hii ni baada ya picha kumuonyesha rapper 21 Savage akiwa amempakata mtoto wa Amber Rose na Wiz Khalifa aitwaye Sebastian mwenye miaka 4 katika ndege binafsi.


Odinga aitisha maandamano kushinikiza mabadiliko

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga
Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, umesema siku ya Jumanne utaongoza maandamano ya wafuasi wake nje ya Ofisi ya Tume ya Uchaguzi jijini Nairobi, kushinikiza mabadiliko ndani ya Tume hiyo kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi mpya wa urais tarehe 26 mwezi Oktoba.

Jennifer Lopez achangia $1m wahanga wa kimbunga Puerto Rico

Jennifer Lopez ameamua kugawana alichokipata katika muziki na wahanga wa Puerto Rico.


Msanii huyo ameamua kuchangia kiasi cha dola milioni moja ambapo ni zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa fedha za kitanzania kwa wananchi hao waliopatwa na janga hilo la kukumbwa na kimbunga cha Maria siku chache zilizopita.

Nilipanda ulingoni nikiwa na msiba wa baba yangu – Campbell

Bondia muingereza, Luke Campbell ametoa ya moyoni juu ya taarifa ya kifo cha baba yake mzazi mzee, Bernard ambaye alifariki dunia kutokana na ugonjwa wa kansa akiwa amefikisha umri wa miaka 58.


Campbell ameeleza kuwa alipata taarifa ya kifo cha baba yake wakati alipokuwa anajiandaa kupambana na Jorge Linares pambano la ubingwa wa WBA na kusema kuwa aliamua kuendelea na maandalizi ya pambano mpaka alipoingia ulingoni hakutaka mtu yeyote kufahamu kilichomkuta.

Jason Derulo alizwa zaidi ya $300k

Msanii wa Marekani Jason Derulo amesherekea wikiendi hii kwa kumwaga machozi.


Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, umeripoti msanii huyo amejikuta nyumba yake iliyopo mjini Los Angeles ikivamiwa na kuibiwa kiasi cha dola 300,000 pamoja na vitu vingine vya thamani kubwa. Hata hivyo msanii huyo hakuwepo nyumbani muda huo.

Panga wagombea CCM lawadia

MWENYEKITI WA CCM, JOHN MAGUFULI.

KAMATI Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) za Chama Cha Mapinduzi (CCM), zinakutana wiki hii katika vikao vya kuchuja majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ngazi za Wilaya.

Mauzo ya’ Sugarcane’ yampagawaisha Tiwa Savage

Mixtape ya ‘Sugarcane’ kutoka kwa mwanadada Tiwa Savage, imeanza kufanya vizuri sokoni ikiwa ni siku chache toka iachiwe.


Mixtape hiyo yenye ngoma sita imekuwa ikiuzwa kwa njia ya mitandao kama Apple Music na iTunes imefanikiwa kushika namba moja kwa mauzo ndani ya muda mfupi.

Monday 25 September 2017

Mfalme Mswati avuta jiko la 14 (+picha)

Mfalme Mswati III wa Swaziland wiki iliyopita ameongeza idadi ya wanawake aliioa na kufikisha 14, kwa kumuoa msichana wa miaka 19.

Mfalme Mswati wa III akiwa na mke wake mpya Siphelele Mashwama nchini Marekani.

Waafrika sasa tumeamka – Dkt Mwakyembe

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amesema kuwa kwasasa Waafrika wameamka na kuamua kurejesha utamaduni wao kwa nguvu zote.


Akizungumza katika Tamasha la Kimataifa la Utamaduni na Sanaa Bagamoyo ambalo limeanza huko Bagamoyo mkoani Pwani, ambalo kwa mwaka huu limeshirikisha wasanii 68 kutoka Tanzania na nje ya Tanzania.

Ripoti: Kundi la P-Square lagawanyika

Kundi la muziki linalowakutanisha ndugu Peter na Paul maarufu kama P-Square limeripotiwa kugawanyika.


Kundi hilo lililofanya kazi kwa zaidi ya miaka mitano linadaiwa kuvunjika rasmi baada ya wawili hao kuingia katika mgogoro mpya. Ripoti iliyowasilishwa na mwanasheria Festus Keyamo kutoka kwa Peter imeonyesha malalamiko kadhaa kwa kundi hilo akiwemo na meneja wao ambaye ni kaka yake Jude.

Rais Donald Trump atofautiana na wanamichezo

Kumekuwa na wamarekani weusi ambao wanapinga sera za Rais mpya, Donald Trump hali ambayo imefikia mpaka wana michezo mbalimbali kuingia katika sakata hilo na kuonyesha hisia zao.


Wachezaji wa timu za Baltimore Ravens na Jacksonville Jaguars za marekani nimiongoni mwa wanamichezo ambao wameonyesha kutofurahia na sera za Trump baada ya kushindwa kuheshimu wimbo wa taifa wa marekani ulipokuwa ukipigwa katika uwanja wa Wimbley ikiwa ni inshara ya kuonyesha umoja wa kumpinga Rais huyo.

Merkel aibuka mshindi

Kansela wa ujerumani , Angela Merkel ameibuka kuwa mshindi katika uchaguzi mkuu nchini humo kwa kipindi cha nne. Hata hivyo mamlaka yake imepungua kutokana na uungwaji mkono mdogo ndani ya chama chake chenye mrengo wa kati kutokana na kuimarika kwa chama cha kulia yaani AFD.

Ukipata bahati ya kutembelea Iran jitahidi kukutana na watu hawa (+video)

Wahenga walisema dunia wawili wawili! ama hakika hawakukosea kabisa kwani hili linakuja kudhihirika huko nchini Iran ambapo watu wawili wamepata umaarufu mkubwa duniani kwa kufanana na wachezaji maarufu duniani, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Lionel Messi na Cristiano Ronaldo

Watu hao wanaofahamiana kwa majina ya Reza Parastesh na Reza Alireza Lou wamefanana na Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ukikutana nao hutaweza kuwatofautisha na mastaa hao.

Reza Alireza Lou na Reza Parastesh

Reza Parastesh yeye alianza kufahamika kupitia mitandao ya kijamii kabla ya vyombo vya habari na nchini Iran wanamuita Messi mwaarabu na umaarufu wake umeenea zaidi barani Ulaya baada ya mashirika makubwa ya utangazaji kumtangaza.


Tayari Parastech ameanza kutoza watu kiasi cha dola $5 kwa kila picha moja utakayopiga nae, na amekiri kuingiza mkwanja kupitia muonekano wake.

Muirani mwingingine ni Reza Alireza Lou yeye amefanana na mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo huyu pia alianza kujulikana kupitia uchaguzi wa mkuu wa Iran uliofanyika mwezi Mei mwaka huu ambapo picha alizopiga na watu waliojitokeza kupiga kura zilisambazwa na vyombo vya kimataifa.

Reza Alireza Lou



Iranians take selfies with Reza Alireza Lou at presidential elections in Tehran.
Guess which football player he resembles? 

Hata hivyo, tayari wawili hao wamekuwa gumzo nchini humo na Vyombo vya Habari na wananchi wakiwapigia upatu kwenye mitandaoni kwa kushinikiza makampuni yawatumie kwenye matangazo.

Kitu cha kushangaza kutoka kwa watu hao ni kwamba wote wanauwezo wa kucheza mpira ingawaje hakuna hata klabu moja iliyojitokeza kuwasajili.

Najua ni kazi sana kukutana na mchezaji kama Lionel Messi au Cristiano Ronaldo ndio maana watu huwa wanaingia hata uwanjani kuwakimbilia kwa hiyo kama ni mtanzania na upo nchini Iran sio mbaya na wewe ukapata selfie na watu hao. Tazama video za watu hao hapa chini








Anna Mghwira atoa agizo Arusha

Mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Anna Mghwira, amemuagiza mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, kufanya mazungumzo na kampuni ya Hodhi ya mali za Reli (Rahco) kuepusha bomoa bomoa eneo la Pasua.

Tarehe / siku nzuri kwa mimba kuweza kutungwa

Leo napenda nizungumzie jambo moja tu ambalo ni juu ya jambo moja tu, nalo ni namna wanavyoweza kui-pin point siku ile ya kilele (i.e fruitful/productive/fertile day), hapa nina maana ya siku ile ambayo wao wanaiita siku ya 14. 

Mbunge CHADEMA amesema ana ushahidi usiotia shaka



Mbunge Arumeru Mashariki (CHADEMA), Joshua Nassari amefunguka na kusema yeye ana ushahidi usiotia shaka juu ya madiwani ambao wamepokelewa jana na Rais kuwa wamenunuliwa na kupewa rushwa na si kuwa wamehama kwa lengo la kukubali kazi anazofanya Rais 

Una Mawe kwenye Figo? Soma hapa

UGONJWA wa mawe kwenye figo siyo mgeni miongoni mwa watu hivi sasa, hasa wenye umri mkubwa. Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni, ukubwa wa tatizo hili umeongezeka, kwani hata vijana wanapatwa na tatizo hili ambalo kitalaamu linajulikana kama ‘Gallstones’.

Le Bron James amtusi rais Trump

Nyota wa mchezo wa mpira wa vikapu nchini Marekani LeBron James amemuita rais wa Marekani 'Bum'{Makalio} kufuatia matamshi aliyotoa kuhusu mchezaji mwenza Steph Curry.

Njia Rahisi Ya Kupata Mimba Haraka Kwa Mwanamke


Kufanya tendo la ndoa mara kwa mara, angalau siku tatu kwa wiki, ikiwezekana on alternate days.
Tumia ovulation prediction kit, hiki ni kifaa ambacho kitakusaidia kujua wakati hasa mwanamke ameengua yai na ndio kipindi ambacho mwanamke ana uwezo wa kushika mimba akikutana na mumewe. Ni rahisi kutumia.

Breaking: Mbunge Peter Msigwa anashikiliwa na Polisi

Kupitia ukurasa wa Twitter wa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, ameandika hivi;-

"Msigwa amekamatwa na Polisi huko Iringa na kushushwa kwa nguvu jukwani ktk Mkutano halali. Msiogope baada ya giza nene asubuhi hutokea!"

Wachina wasepa na ngoma za Mrisho Mpoto

Ngoma ambazo zilikuwa zinatumiwa na msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto katika maonyesha ya Utalii Duniani yaliyofanyikia nchini China zimegombaniwa na baadhi ya wachina waliojitokeza katika maonyesho hayo. 

Pogba kutibiwa na Daktari wa Barcelona

Nyota wa Manchester United Mfaransa Paul Pogba huenda akafanyiwa upasuaji na daktari kutoka Finland Sakari Orava ambaye amefanikisha upasuaji wa winga wa Barcelona Ousmane Dembele.