Tuesday 26 September 2017

Mwanamke mnene na mzito zaidi duniani ‘Eman Ahmed’ afariki dunia

Mwanamke mnene na mzito zaidi duniani, Eman Ahmed amefariki dunia leo mjini Abu Dhabi katika hospitali ya Burjeel alikokuwa akipata matibabu ya kupunguza unene.

Eman Ahmed akiwa amelazwa katika Hospitali ya Burjeel siku chache kabla ya kifo chake.

Eman (37) raia wa Misri amefariki leo akiwa na uzito wa kilo 501 sawa na nusu tani ambapo wazazi wake wamesema unene wa mtoto wao ulianza tangia akiwa mdogo na hajawahi kutoka nyumbani kwa miaka 17 wala kutembea tangia azaliwe hadi anakufa.

Jopo la madaktari 20 waliokuwa wakipigania uhai wa Eman wamesema amekufa baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo ili aendelee na matibabu mengine.

Taarifa za awali kutoka kwa Madaktari hao wamesema Eman anasumbuliwa na matatizo ya Figo na ugonjwa wa Matende ambao ulimuanza tangia akiwa mdogo.

Eman alisafirishwa mwezi Februari kutoka Misri na kwenda India na kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kwanza ambapo madaktari katika hospitali ya Saifee mjini Mombai walifanikisha kupunguza kilo 230 kabla ya kumsafarisha kwa ndege ya mizigo mwezi Mei mwaka huu kumpeleka Uarabuni ambako mauti yamemkuta akiwa na uzito wake wa awali.

Katika maisha yake Eman hajafanikiwa kupata mtoto, Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema.