Tuesday 26 September 2017

Mauzo ya’ Sugarcane’ yampagawaisha Tiwa Savage

Mixtape ya ‘Sugarcane’ kutoka kwa mwanadada Tiwa Savage, imeanza kufanya vizuri sokoni ikiwa ni siku chache toka iachiwe.


Mixtape hiyo yenye ngoma sita imekuwa ikiuzwa kwa njia ya mitandao kama Apple Music na iTunes imefanikiwa kushika namba moja kwa mauzo ndani ya muda mfupi.

Kupitia mtandao wa Instagram mrembo huyo ameshukuru mashabiki zake kwa kumsapoti na kuandiaka “Baba God, you too mush  #SugarCaneEP #SMD #323ENT #ROCNATION#SavageSoldiers.”


Ukianchana na ngoma ya ‘Sugarcane’ inayobeba mixtape hiyo kuna ngoma kama ‘Ma Lo’ aliyomshirikisha Wizkid na Spellz, ‘Get It Now’, ‘Me & You’ na ‘Hold Me Down’ na inapatikana kwa kiasi cha dola 5.94 sawa na kiasi cha shilingi 13,327.53 za kitanzania.