Tuesday 26 September 2017

VIDEO: Daktari wa Manji Utotoni Afunguka Mahakamani

Leo Septemba 25, katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam, ambapo mahakama hiyo imeanza kuisikiliza kesi ya Siku tatu mfuliulizo ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili mfanyabiashara Yusuf Manji mbele ya hakimu mkazi Cyprian Mkeha.


Upande wa utetezi wa Manji wakiongozwa ba wakili Hajra Mungula ulileta mashahidi 3 ambapo shahidi wa Kwanza alikuwa ni Manji mwenyewe, na wapili alikuwa ni Daktari wake anayemtibu katika Hospitali ya Aghakan Jijini humo na watatu kwa siku ya leo alikuwa ni Daktari wake aliyemtibu manji tangu akiwa na umri wa miaka 3. 


Shahidi huyo watatu aliyejitambulisha kwa jina la Daktari Khani ameieleza mahakama kuwa amekuwa daktari familia ya Manji tangu 1978.


Na kwamba Manji amekuwa mgonjwa wake kwa muda wote na amekuwa akiwasiliana na yeye mara 3 hadi 4 kwa mwaka.


Licha ya matatizo ya kawaida ambayo amekuwa akimtibu pia amesema anafahamu Yusuf Manji ana tatizo la moyo ambalo aliwahi kumweleza.


Wakili wa Serikali Timon Vitalis : alimtaka Daktari aiambie mahakama kama Manji anatumia dawa za kulevya.


Ambapo alijibu Katika kipindi chote hajawahi kubaini kama anatumia dawa hizo.


"Mara kwa mara nimekuwa na muwekea Dripu dawa ila sijawahi kuona kama kuna dalili zote... natambua ana tatizo la moyo na hata baba yake alikuwa nalo pia ingawa alifariki kwa Saratani" Alisema.


Kwa upande wake Yusuf Manji akiwa kama shahidi ameileza mahakama Kuwa anashangaa katika tuhuma za dawa kukevya wapelelezi walichukua Simu yake moja, Saa, Kompyuta na Kadi ya Benki (Credit Card) na kwamba mpaka sasa bado havijarudishwa


Baada ya kusikiliza ushahidi huo Hakimu Cyprian Mkeha ameiharisha kesi hiyo mpaka kesho Septemba 26, 2017 majira ya saa tatu asubuhi.


TAZAMA FULL VIDEO HAPO CHINI