Monday 25 September 2017

Diamond aamua kuwajibu mashabiki wanaomtusi mtandaoni

Katika hali ya kushangaza Diamond Platnumz amewatolea lugha chafu baadhi ya mashabiki zake ambao walikuwa wakimsema hasa kutokana na sakata lake na Hamisa Mobetto iliyotokea katikati ya wiki hii.

Katika posti aliyoweka katika mtandao wa Instagram ambayo ilikuwa ya Zari akimtakia heri katika siku yake ya kuzaliwa, baadhi ya mashabiki walianza kuponda na kumsema, kitendo kilichomkera Diamond na kuamua kuwajibu kwa lugha kali.

“Picha zako tu zinaonesha… alafu design kama unatafuta mabwana insta,” aliandika Diamond akimjibu moja ya shabiki.

“Baba yako mwenyewe anaonekana ana michepuko kila mtaa,” aliongeza na kumaliza kwa tusi,” aliandika Diamond.