Monday 25 September 2017

Ukipata bahati ya kutembelea Iran jitahidi kukutana na watu hawa (+video)

Wahenga walisema dunia wawili wawili! ama hakika hawakukosea kabisa kwani hili linakuja kudhihirika huko nchini Iran ambapo watu wawili wamepata umaarufu mkubwa duniani kwa kufanana na wachezaji maarufu duniani, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Lionel Messi na Cristiano Ronaldo

Watu hao wanaofahamiana kwa majina ya Reza Parastesh na Reza Alireza Lou wamefanana na Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ukikutana nao hutaweza kuwatofautisha na mastaa hao.

Reza Alireza Lou na Reza Parastesh

Reza Parastesh yeye alianza kufahamika kupitia mitandao ya kijamii kabla ya vyombo vya habari na nchini Iran wanamuita Messi mwaarabu na umaarufu wake umeenea zaidi barani Ulaya baada ya mashirika makubwa ya utangazaji kumtangaza.


Tayari Parastech ameanza kutoza watu kiasi cha dola $5 kwa kila picha moja utakayopiga nae, na amekiri kuingiza mkwanja kupitia muonekano wake.

Muirani mwingingine ni Reza Alireza Lou yeye amefanana na mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo huyu pia alianza kujulikana kupitia uchaguzi wa mkuu wa Iran uliofanyika mwezi Mei mwaka huu ambapo picha alizopiga na watu waliojitokeza kupiga kura zilisambazwa na vyombo vya kimataifa.

Reza Alireza Lou



Iranians take selfies with Reza Alireza Lou at presidential elections in Tehran.
Guess which football player he resembles? 

Hata hivyo, tayari wawili hao wamekuwa gumzo nchini humo na Vyombo vya Habari na wananchi wakiwapigia upatu kwenye mitandaoni kwa kushinikiza makampuni yawatumie kwenye matangazo.

Kitu cha kushangaza kutoka kwa watu hao ni kwamba wote wanauwezo wa kucheza mpira ingawaje hakuna hata klabu moja iliyojitokeza kuwasajili.

Najua ni kazi sana kukutana na mchezaji kama Lionel Messi au Cristiano Ronaldo ndio maana watu huwa wanaingia hata uwanjani kuwakimbilia kwa hiyo kama ni mtanzania na upo nchini Iran sio mbaya na wewe ukapata selfie na watu hao. Tazama video za watu hao hapa chini