Monday 25 September 2017

Wahukumiwa kwenda jela miaka 22 kwa dawa za kulevya

Abbas Kondo na Albeto Mandes wamehukumiwa kwenda jela miaka 22 kila moja kwa kosa la kujihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya cocaine na heroin. Washtakiwa hao ambao walitenda makosa yao kwa nyakati tofauti walihukumiwa pia kulipa faini ya jumla ya Sh320.7 milioni.

Hukumu ya Kondo ilitolewa katikati ya wiki na Jaji Korosso.

Kondo ambaye ni mkazi wa Mmtaa wa Lindi wilayani Ilala alikamatwa Mei 14, 2011 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akitokea Sao Paulo, Brazil akiwa na kete 77 za cocaine zilizokuwa na thamani ya Sh58,588.000. Mendes ambaye ni raia wa Guinea Bissau alikamatwa Aprili 15, 2012 katika uwanja huo akiwa na gramu 1,277 za heroin zilizokuwa na thamani ya Sh57,483.000 akielekea nchini Mali. Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Mfawidhi Matogolo.