Tuesday 26 September 2017

Video: Diamond na Zari wamekomesha ‘choko choko’


Siku ya Jumamosi ilikuwa ni siku ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Zari mzazi mwenzake na Diamond Platnumz.


Shughuli hiyo ilifanyika nchini Afrika Kusini, huku habari zikizagaa kuwa Diamond hawezi kwenda kuungana na mrembo wake huyo baada ya hivi karibuni kukiri kuchepuka na mwanamitindo Hamisa Mobeto na kuzaa naye mtoto wa kiume [Dylan].

Hata hivyo hali iligeuka tofauti baada ya first lady wa Madale kuonekana katika video zilizosambaa mitandaoni akisherekea siku yake hiyo muhimu akiwa na Diamond huku wakiwa katika mahaba motoo.

Kupitia tukio hilo tumeweza kufahamu zaidi maana ya wimbo wa ‘Eneka’ ulipotokea kwani wamedhihirisha mapenzi yao ni ‘Strong’ na wapo tayari kukabiriana na kila hali kama chombo kinaposafiri baharini.

Video Player
00:00
00:08
Video Player
00:00
00:14

Kwa picha na video zilizosambaa unadhani penzi la Diamond na Zari litakufa kirahisi rahisi hivyo? au ndio drama za mitandaoni?