Friday 22 September 2017

Utafiti: Kufanya Mazoezi Kunasaidia Kuimarisha Nguvu Za Kiume

Habari njema kwa wanaume wenye tabia ya kufanya mazoezi, na sababu nzuri kwa wale wasiofanya kuanza kufanya mazoezi. Wanaume wanaofanya mazoezi kwa kati ya masaa matatu mpaka matano kwa wiki wanauwezekano mdogo wa kupata matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume kuliko wasiofanya kabisa. utaafiti mkubwa iliyofanyika katika chuo kikuu cha Havard nchini marekani umebaini.

Utafiti huo uliojulikana kwa jina la Havard Health professionals Follow-up Study (HPFS), ulichapisha matokeo hayo katika jarida la kisayansi linalojulikana kwa jina la ’’Annals of Internal Medicine`` mwezi wa nane mwaka 2003

Magonjwa ya moyo hujionyesha kwa kupungua kwa nguvu za kiume.
Mfumo wa moyo na mishipa ya damu ndio unaohusika haswa na nguvu za kiume. Kitu kingine kinachohusika na nguvu za kiume ni homoni ijulikanayo kama testosterone, ambayo mara nyingi hujulikana kama homoni ya kiume. Kwa maana hiyo basi matatizo ya moyo na mishipa ya damu huanza kujionyesha mapema kama upungufu wa nguvu za kiume.

Kushuka kwa kiwango cha homoni ya testosterone ambacho hutokea kadiri umri unavyoongezeka pia huchangia kusababisha upungufu wa nguvu za kiume. Mazoezi, hususani kutembea, kukimbia, kuendesha baiskeli na mazoezi mengine yanayoufanyisha moyo kazi hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo na hivyo kusaidia mzunguko wa damu. Mazoezi pia husaidia kuongeza kiasi cha homoni testosterone.

Wanaume wangi wako kwenye hatari ya kupata upungufu wa nguvu za kiume.
Utafiti mkubwa uliohusisha zaidi ya wanaume 31,000 ambao hawakuwa na saratani ya tezi ya prostate (prostate cancer), ulionyesha kwamba theluthi moja ya wanaume hao waliwahi kupata upungufu wa nguvu za kiume.

Uwezekano wa tatizo hili unaongezeka kadiri umri unavyoongezeka. Utafiti huu pia ulionyesha kwamba, mazoezi yanaweza kuongeza muda wa mwanaume wa kawaida kuendelea kuwa na nguvu za kawaida za kiume kwa zaidi ya miaka kumi. Tafiti zilizopita zimeonyesha mazoezi yanaweza pia kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tezi ya prostate, ambayo matibabu yake huweza kusababisha kupoteza nguvu za kiume.

Sababu zingine zinazoweza kusababisha kupungukiwa kwa nguvu za kiume. Tofauti na kutokufanya mazoezi, sababu zingine zinazoweza kubadilishwa ambazo pia huongeza uwezekano wa kupungukiwa kwa nguvu za kiume ni pamoja na uvutaji sigara, na unene uliokithiri. Kujenga tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara na kula chakula bora kunaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa sana katika kujikinga na tatizo hili.

Ni wakati muafaka wa kuchukua uamuzi na kujenga tabia ya kufanya mazoezi, na kula chakula bora.