Tuesday 26 September 2017

Wiz Khalifa amemruhusu 21 Savage kuwa baba mlezi?

Ule usemi wa ukipenda boga penda na ua lake, upo mpaka mbele hii ni baada ya picha kumuonyesha rapper 21 Savage akiwa amempakata mtoto wa Amber Rose na Wiz Khalifa aitwaye Sebastian mwenye miaka 4 katika ndege binafsi.



Picha hiyo imeweka na rapper huyo kupitia mtandao wa kijamii wake Instagram. Kuonyesha penzi ni la moto na tamu inaelezwa kuwa miezi michache iliyopita Amber alimnunulia mpenzi wake huyo pete ya iliyoandikwa ‘Loyality 21’ kama ishara ya uaminifu, pete hiyo yenye almasi, dhahabu na madini mengine yapatayo 1,100.

Pia wawili hao waliwahi kunaswa na kamera za TMZ, wakiwa wanaelekea nyumbani kwa 21 kwa ajili ya utambulisho kwa familia yake. Swali ni je?, Wiz Khalifa ameridhia 21 Savage kuwa baba mlezi kwa mwanaye au ndo yakina Future na Ciara.