Wednesday 25 October 2017

Kifafa cha Mimba (Preeclampsia, eclampsia)

Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaohusiana na msukumo mkubwa wa damu (high blood pressure) wakati wa ujauzito pamoja na kuharibika kwa viungo muhimu mwilini kama vile figo na ini. Kwa kawaida ugonjwa huu hutokea baada ya nusu ya kwanza ya ujauzito kuisha (kuanzia wiki ya 20 au miezi mitano ya ujauzito).

Tabia Hii Moja Itakufanya Uendelee Kuwa Masikini Maisha Yako Yote

Kila siku huwa najifunza sana kuhusu fedha na kuhusu tabia za watu kuhusu fedha. Pia nimekuwa nakazana sana kujifunza kuhusu fedha katika miaka mingi iliyopita. Nimekuwa najifunza kuhusu historia ya fedha, historia ya matajiri mbalimbali waliopata kuwepo kwenye uso huu wa dunia. Na muhimu zaidi nimekuwa najifunza kupitia tabia za wengine

Zijue sababu zinazopelekea wapenzi wengi kuchokana mapema

Hivi uliwahi kujiuliza hivi ni kwanini baadhi ya mahusiano ya kimapenzi hufa mapema, kama si kufa basi kushuka kwa mahusiano hayo? Moja kati ya sababu ambayo husababaisha kufa kwa mahusiano ni ile tabia ya kuchokana mapema katika mahusiano na moja kati ya sababu kubwa ambayo hupelekea kuchokana mapema ni:

Harmorapa afunguka kuhusu kupotea kwake

Msanii ambaye hakauki vituko mitandaoni Harmorapa, amewajibu watu wanaomsema kuwa amepotea pamoja na kiki zake zote, na kusema kwamba hajapotea isipokuwa yuko busy na biashara.

SIMULIZI: DADA VUA 13


..........ilipoishia

Huku kwa kina Helena tayari Lucy alisharejea katika hali yake ya kibinadamu na wakati huohuo Sule alionekana anaondoka.Kwa kuwa helena alikuwa amepewa kazi ya kumzuia sule asiondoke bila kunywa kinywaji kile alichopewa na Shangazi,Basi alimfuata sule akiwa na kile kinywaji kujaribu kama hilo litawezekana.....

Odinga amvaa Afisa mkuu IEBC Kenya

Kiongozi wa Muungano wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga amesema Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume Huru wa Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ya nchini Kenya Ezra Chiloba bado yupo ofisini ingawa alisema kuwa amechukua likizo na asingeshiriki katika uchaguzi.

Wakenya kupumzika siku ya Jumatano

Serikali ya Kenya imetangaza kuwa siku ya Jumatano itakuwa ya mapumziko ili kuwapa wananchi muda wa kutosha kwa maandalizi ya uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika Alhamisi ya Oktoba 26.

Waethiopia 74 wakamatwa Mtwara

Mtwara. Ofisi ya Uhamiaji mkoani Mtwara kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) imewakamata wahamiaji wasiofuata utaratibu 74 raia wa Ethiopia.

Mabalozi wainyooshea kidole Kenya

Nairobi, Kenya. Mabalozi wa nchi za Ulaya na Marekani wamezungumzia “kuzorota kwa mazingira ya kisiasa” katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa marudio na wakahimiza vyama vikuu kujizuia kufanya uchochezi na kuacha kuzikashfu taasisi.

Polisi wakamata Wapinzani

Wafuasi kadhaa wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, wamekamatwa jana Jumapili mjini Lubumbashi walipokuwa wakihudhuria mkutano wa maandalizi ya kuwasili kwa kiongozi wa chama cha UDPS, Felix Tshisekedi, katika katika mji huo.

Everton Waifuata Chelsea Kwa Treni

Wayne Rooney akiwa na wachezaji wenzake wa Everton kwenye stesheni ya treni leo kwa safari ya London kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Carabao dhidi ya wenyeji, Chelsea kesho ambao utakuwa wa kwanza kocha wa muda, David Unsworth aliyepewa nafasi ya Ronald

Mawaziri na Wabunge kuanza kupewa tuzo

Kamati ya utawala ya shindano la tuzo za utekelezaji maendeleo kwa kasi ya juu kwa Wabunge na Mawaziri (THSDA) imezindua shindano la kutoa tuzo kwa Wabunge na Mawaziri watakaofanya vizuri katika kutekeleza majukumu ya kuwaletea Wananchi maendeleo.

Niyonzima awapa neno mashabiki wa Simba

KIUNGO nyota wa Simba inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, Mnyarwanda Haruna Niyonzima, amesema mashabiki wa timu hiyo wajiandae kumuoa "Niyonzima mpya" baada ya muda mfupi.

Kizimbani kwa kutishia kumuua Diwani

WATU nane wakazi wa Ntyuka Manispaa ya Dodoma, wamefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo ya Chamwino kwa tuhuma za kutishia kumuua kwa maneno Diwani wa Kata ya Ntyuka, Theobale Emmanuel.

Watumishi wala rushwa watangaziwa kiama

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Kapteni mstaafu George Mkuchika
Dar es Salaam. Serikali imesema mtumishi anayefanya kazi katika Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita) akibainika kushiriki vitendo vya rushwa atachukuliwa hatua mara moja.

Afisa wa TRA apandishwa kizimbani kisa kumiliki mali zisizolingana na kipato chake

Afisa Msaidizi wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jennifer Mushi amepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kosa la kumiliki mali ambazo ni magari 19 na kuishi maisha ya kifahari kinyume na mshahara wake.

Mshtakiwa amesomewa makosa yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi na Wakili wa Serikali, Vitalis Peter ambaye alidai mshtakiwa ana makosa mawili.

Darassa kuamsha dude la kufungia mwaka

Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Darassa amezungumzia ujio wake mpya.

Rapper huyo ambaye mara mwisho alisikika na ngoma ‘Hasara Roho’ ameiambia Dj Show ya Radio One yupo katika maandalizi ya kufanya hivyo ila kwa sasa asingependa kulizungumzia sana kwani yeye siku zote siyo muongeaji zaidi ya kazi.

Tuesday 24 October 2017

SIMULIZI: SHANIA PART 02 EP 05


..........iilipoishia

Mike alimwambia"Mmmmmh kazi mnao lakini wewe ulikuwa unatakaje"......Pacha wa Shaina alijitengenezea koo vizur"mh!!mh!!! mike jomouny kwanini unakuwa mgumu kunielewa"......Mike alimwambia "Oukey nimeshakuelewa twende kwanza Huko dukani tukirudi tutaongea vizuri.Shania alijipa ushindi mkubwa na kujisemea kimoyo moyo" Yeees!!"kisha

Hawa ndio wachezaji 24 wa Taifa Stars waliochaguliwa kucheza na Benin

Leo Jumanne kocha wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Salum Mayanga ametangaza kikosi cha wachezaji 24 ambacho kitacheza na timu ya taifa ya Benin Novemba 11 ya mwaka huu.


Kikosi hicho kilichotangazwa na mwalimu Mayanga ni pamoja na magolikipa Aishi Manula, Peter Manyika na Ramadhan Kambwili.

Wasanii Bongo kufanya siri mauzo ya albamu, Ben Pol afunguka

Mkali wa muziki wa RnB Bongo, Ben Pol amefunguka utamaduni wa wasanii kutoa albamu lakini wanakuwa wasiri katika mauzo na idadi kamili ya copy.


Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Kidume’ ambayo amemshirikisha Chidnma kutoka nchini Nigeria, ameiambia East Africa Radio kuwa ni kweli hilo lipo ila kwa upande wake hadhani kama lipo kutokana albamu yake ya kwanza alitoa akiwa chini ya record label.

Rekodi za Emmanuel Okwi katika Uwanja wa Uhuru hizi hapa

Zikiwa zimesalia siku chache kuelekea katika mtanange wa watani wa jadi, Yanga SC ambao ndiyo wenyeji wa kiwakaribisha Simba SC katika Uwanja wa Uhuru Octoba 28 mwaka huu mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara.


Hizi ndizo rekodi chache tu za mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda na klabu ya Simba, Emmanuel Okwi katika Uwanja wa Uhuru toka sajiliwe msimu huu.

Kilichojiri Kesi ya Lulu Mahakamani leo. Mke wa Dk Slaa akosekana ushahidi (+Audio)

Shahidi wa pili upande wa utetezi ambaye ni mke wa Dk Slaa, Josephine Mushumbushi, na pia aliyekuwa mmoja wa madaktari wa marehemu Kanumba, ameshindwa kufika mahakamani Jumanne hii kwa ajili ya kutoa ushahidi wake kutokana na sababu zilizoelezwa kuwa yupo nje ya nchi na hakuweza kupatikana moja kwa moja.


Akiongea na waandishi wa habari baada ya kesi hiyo kuahirishwa, mtaalamu na mfuatiliaji wa kesi hiyo amesema, “Mwanzoni wakati anasomewa maelezo ya awali walisema

Ronaldo, Messi wakumbatiana kwa bashasha usiku wa tuzo za FIFA (Picha)

Katika tuzo zilizotolewa hapo jana siku ya Jumatatu usiku katika Jiji la London mastaa wengi walihudhuria wakiwemo waigizaji lakini tukio kubwa lililovutia ni kukutana na kukumbatiana kwa Cristiano Ronaldo na Leonel Messi.


Mchezaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akisalimiana na kukumbatiana na Leonel Messi wa Barcelona

Mitandao ya Facebook, LinkedIn yaongoza kwa kuvunja ndoa za watu

Mitandao ya kijamii ya Facebook na LinkedIn inaongoza kwa kuvunja ndoa za watu duniani kwa wanandoa kuwa na mahusiano na watu zaidi ya mmoja mitandaoni.


Hayo yamesemwa na Mwanasheria Abigail Lowther, kutoka katika kituo cha Wanasheria cha Hall Brown Law Family cha nchini Uingereza.

La Liga yatawala kikosi bora cha FIFA

Katika tuzo zilizotolewa hapo jana siku ya Jumatatu usiku jumla ya wachezaji watano wa klabu ya Real Madrid wametajwa katika kikosi kinaunda wachezaji 11 wa FIFA.


Kikosi bora kilichotangazwa na FIFA 2017

Ronaldo, Zidane wang’ara tuzo za FIFA (Picha)

Mshambuliajia wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amelitetea tena taji lake la mwanasoka bora wa Fifa kwa mwaka wa pili mfululizo.


Ronaldo amemshinda Lionel Messi ria wa Argentina anayekipiga Barcelona aliyeshika nafasi ya pili.

Mambo 6 Ambayo Mjasiriamali Anatakiwa Kuyafanya Kila Siku

Kati ya kitu ambacho kila mjasiriamali mwenye nia ya kufanikiwa anacho ni kule kutaka kuona anakifikia mafanikio makubwa ya kibiashara. Lakini pamoja na kuwa na nia hiyo ya kufikia mafanikio hayo, mjasiriamali huyu hawezi kufanikiwa mpaka ajue mambo ya msingi yanayoweza kumsaidia kufanikiwa na kuyafanya karibu kila siku.

Tujiepushe Kunywa Maji Baridi Yana Madhara Kwa Afya Ya Binadamu

MADHARA YA KUNYWA MAJI BARIDI
UNYWAJI wa maji baridi, hasa katika joto kali kama la Dar es Salaam, ni kiburudisho kikubwa cha koo na huleta faraja kubwa mwilini. Ni jambo la kawaida pia kwa mtu kuhitaji kunywa maji hayo mara baada ya kula mlo, iwe mchana au usiku.

Gavana mteule afunguka

Dar es Salaam. Gavana mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga amesema amepokea kwa heshima kubwa dhamana aliyopewa na Rais John Magufuli na anatambua changamoto za nafasi hiyo.

SIMULIZI: DADA VUA 13


..........ilipoishia

Huku kwa kina Helena tayari Lucy alisharejea katika hali yake ya kibinadamu na wakati huohuo Sule alionekana anaondoka.Kwa kuwa helena alikuwa amepewa kazi ya kumzuia sule asiondoke bila kunywa kinywaji kile alichopewa na Shangazi,Basi alimfuata sule akiwa na kile kinywaji kujaribu kama hilo litawezekana.....

Kocha wa timu ya Taifa ya Sweden atua Nchini

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya wanawake ya Sweden, Mariane Sundhage leo Oktoba 23, 2017 amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Stephen Kebwe katika Ofisi ya Mkoa na kufanya mazungumzo yenye lengo la kuboresha soka la wanawake nchini.

Bei ya korosho yazidi kunona. Lindi

Bei ya korosho yazidi kunona.Na.Ahmad
IKIWA ni mnada wake wa kwanza kufanyika katika msimu wa 2017/2018,chama kikuu cha ushirika cha RUNALI mkoani Lindi, jana kilifanikiwa kuuza korosho kwa bei ya juu kuliko bei za juzi zilizonunuliwa zao hilo katika chama kikuu cha Lindi Mwambo.

Dalili za Ugonjwa wa zinaa - kisonono

Kisonono ni ugonjwa wa zinaa unaoambukizwa, ugonjwa huu hutokana na wadudu aina ya Neisseria gonorrhoeae. Ugonjwa huu pia huambukizwa kwa tendo la ngono na hata kutoka kwa mama mjamzito anapojifungua huweza kumuambukiza pia mtoto endapo atakuwa alikuwa nao.