Tuesday 24 October 2017

Diego Maradona hakufurahia kumkabidhi tuzo Ronaldo

Habari kubwa jana na leo ni kuhusu Cristiano Ronaldo, Mreno huyo amefanikiwa kutwaa tuzo ya The Best Fifa Player Of The Year 2017 ikiwa ni mara ya pili mfululizo na akimbwaga mpinzani wake mkubwa Lioneil Messi.

Katika utoaji wa tuzo hizo usiku wa jana mjini London gwiji wa Argentina Diego Maradona alitoa tuzo ya mchezaji bora wa kiume iliyokwenda kwa Cr7 na Maradona kukiri kutofurahia jambo hilo.

Maradona anasema angefurahi kama tuzo hiyo asingeimkabidhi Cristiano Ronaldo na badala yake angemkabidhi Muargentina mwenzake Lioneil Messi ambaye naye alikuwepo katika usiku wa tuzo hizo.

Maradona ambaye aliwahi kuwa kocha wa Lioneil Messi katika timu ya taifa mwaka 2008 na 2010 amesema jambo la kumpa Ronaldo tuzo hiyo lilikuwa likimuumiza roho wakati akitekeleza suala hilo.

Lakini Maradona amekiri kufurahia kuonana na Lioneil Messi kwani wawili hao walitajwa kuwa na msuguano jambo ambalo lilithibitika zaidi pale Messi alipomtosa kadi ya mualiko Maradona katika harusi yake.

Maradona alimponda Messi kwa kutokuwa kiongozi bora wa timu ya taifa lakini usiku wa jana amekiri kwamba Muargentina huyo ni muhimu kwa timu yao ya taiafa na atakuwa bora kwa muda mrefu zaidi.