Monday 23 October 2017

SIMULIZI: SHANIA PART 02 EP 4


...........iilipoishia

Mike na wenzake walianza kupata mwanga kwa kile alichokizungumza Shania kwani kwa kiasi fulani kina ukweli ndani yake.Shania alionekana akitetemeka kwa baridi ndipo Lois alipovua shati lake na kumvalisha Shania.Shania alishukuru sana kwa kitendo cha Lois kumsitiri"Waooooh!!! Asante sana wangu".Wakati wanakaribia ufukweni ghafla upepo mkali ulianza kuvuma Shania aliwaambia"Baba yangu atapita hapa sasa hivi"...

Songa nayo......LEO NATAKA SHARE TUU ZIKIFIKA HATA SASA HIVI NAACHIA INAYOFUATA.

Kimya na woga kilitawala pale mara baada ya Shania kutoa taarifa kuwa Baba yake anapita maeneo hayo.Mike aliikumbatia bible vizuri akiamini ya kwamba atashuhudia kile alichoambiwa na Shania.Shania alipepesa macho huku na kule kwa kuangalia juu ili amuone Baba yake,Ukweli ni kwamba Shania bado yupo kikazi na hapo alipo alikuwa anawarubuni kina Mike ili tuu aweze kuwaweka mtegoni.Upepo ulivuma mkali sana mara ghafla kukatulia tuuli!!!,Mike alimtazama Shania machoni ili agundue ni uelekeo upi anapotaza naye atazame.Mike aligundua ni wapi anatazama ndipo Mike aliponena na mungu,Mike aligeuza macho kule anakotazama Shania.Kina Lois walikuwa wameduwaa tuu kuona Shania anavyoshangaa kwa kuelekeza macho sehemu moja.

Mike baada ya kutazama kule alipokuwa anatazama Shania aliona taswira ya mtu lakini kama vile ana kiwili wili cha mnyama mwenye manyoya mengi san.Mara ghafla alishuhudia lile sanduku walilokuwa wakilitumia kwa kuwahifadhi kina Lois likishushwa maeneo ya pale walipo.Mike aliingiwa wasi wasi sana huku akijisemea kimoyomoyo"Sasa hapa nitajua mchezo mzima huyu Shania akinidanganya tuu kuhusu hili nitajua ya kwamba tuko mtegoni"Sanduku lile lilitumbukia kwenye maji na walioona ni Shania na mike japokuwa Shania anajua ni yeye tuu aliyeona tukio lile.Upepo mkali ulivuma kwa mara nyingine kisha ile taswira ikapotea "vuuuph!!!!" Shania alirudisha macho yake na kuwatazama kina Lois,Wakati huo mike alijikausha kama vile hajui kitu.

Shania alianza kuongea"Baba yangu kapita sema ana safar zingine"......Mike alimuuliza"Sasa mbona upepo ulikuja kisha ukatulia halafu ukaja tena kwanini"......Shania alimtazama mike akajua tuu hapa huyu mshenzi kashajua kilichokuwa kinaendelea.

YAANI NDUGU MSOMAJI SHANIA AMEAMUA KUTUMIA AKILI SANA KUWATEKA HAWA KINA MIKE LAKINI MIKE PIA YUKO MAKINI SANA HIVYO HII GAME NI NGUMU SANA.

Shania alitabasamu kisha akamwambia"Kamanilivyowaeleza baba yangu anataka niwapeleke na hapa alipokuja aliniletea kifaa cha kuwabebea nyie,Mbali na hivyo ndani ya hicho kifaa kuna mali nyingi ambazo ni dhahabu za kuwadanganyia nyie ili muingie mtegoni".Yaani Shania anataka ajiaminishe kwa kina Mike ila nia yake ni kuwachukua kiukweli ukweli.Mike alimuuliza"Kwa hiyo hizo dhahabu ni za kweli au ni miujiza?"......Shaina alicheka cheko moja la kutamanisha"hahaaahaa!!! hizi dhabu ni za ukweli lakini kuzitumia zinahitaji masharti sana hata binadamu wa kawaida anaweza kuzitumia ila kuna mambo anatakiwa kuyafanya iliazitumie".Kina Dean walipata mshangao haswaa wakajikuta wote wameuliza swali moja kwa wakati mmoja"Masharti gani hayo!!??"

Shania alishajua kuwa kuna baadhi yao walikuwa wana tamaa hivyo ni rahisi yeye kuwateka.Aliwajibu",Mmmmh mbona mmeuliza kwa mshangao mnazitaka au??"........Lois alijibu kwa niaba yao"no!no! sio kwamba tunazitaka bali tunahitaji kujua masharti yake tuu na sio kingine"........Shania aliwakata kauli"Mmmh!! Tuachane na hayo mambo bwana".Wakati yoote yanaendelea mtumbwi ulikuwa ukisonga mbele kuelekea ufukweni.Ndani ya dakika 15 tayar walishafika nchi kavu na moja kwa moja waluelekea kunako nyumba waliyofikia kina Mike.Walifika ndani wakiwa pamoja na Shania kisha wakaanza kufanya ustaarabu wa kula.Dean aliwaambia"Hey mazee mnajua kuwa hapa umebaki unga tuu mchele umekwisha"........Mike alimjibu"Kwani si tunaondoka kesho haina shida tukila ugali leo".Shania aliwatazama kisha akawauliza"Kwani nyie mlikuwa mnataka kula nini leo??".......Lois alidakia"Shania unajua sisi tumezoea mapochopocho kama vile tambi,Matunda na vinywaji vinywaji".......Lois alijibu kama utani kisha wakacheka wote "Hahaaaaaa".

" Oukey sasa sikieni nataka mmoja wenu tuende supermarket tukachukue vitu vya kuja kutumia kwa siku ya leo na kesho kabla hamjaondoka".........Majamaa walitazamana kuona nani yuko tayar kwenda na Shania.Lakini kwa jinsi Shania alivyoongea wote walitokea kumuamini kuwa hana shida tena,Mike alisema"Wacha mi niende naye nyie endeleeni kuwaparua hawa samaki.Shania alimwambia Mike sasa ngoja nikachukue pesa mahali nakuja ndani ya dakika 5 tuu.Walimsubiri kweli hazikuisha dk 10 alirudi akiwa na kipochi kisha akawafunulia ile pochi.Ilikuwa imejaa mipesa sana,Basi mike na Shania moja kwa moja walielekea barabarani ili wapate kausafiri.Walipofika njiani Shania alimsimamisha mike"Miike nikuambie kitu?"....."Eeeheee!!"........."Mike bwaaana mi sitaki kurudi kule waliko baba yangu na Shaina"......Shania aliongea kwa sauti tamuu huku akijibaraguza kwa Mike"Halafu mike kitu kingine unajua sisi kule hatuna uhuru kabisa yaani kuna vitu tunatamani lakini hatuwezi kupata"........Mike alimuuliza"Kitu gani hicho ambacho hampati?".........Shania alinena maneno fulani kimoyomoyo kisha akamjibu"Unajua sisi binadamu tumeumbwa kutamani na kupenda,Basi kuna wakati huwa napata hamu ya kuwa na mwanaume lakini kulingana na mazingira inakuwa ni ngumu"....Yaani Mike siku zote huwa hapendi kusikia maneno kama hayoa lakini kulingana na Shania alivyojipanga alimfanya Mike kutokuwa na hofu juu yale yaliyotokea kipindi cha nyuma.cha kushangaza zaid hata bibilia hatumii kama alivyokuwa anaitumia kipindi cha nyuma.

Mike alimwambia"Mmmmmh kazi mnao lakini wewe ulikuwa unatakaje"......Pacha wa Shaina alijitengenezea koo vizur"mh!!mh!!! mike jomouny kwanini unakuwa mgumu kunielewa"......Mike alimwambia "Oukey nimeshakuelewa twende kwanza Huko dukani tukirudi tutaongea vizuri.Shania alijipa ushindi mkubwa na kujisemea kimoyo moyo" Yeees!!"kisha akamwambia"Sawa mike naomba unisaidie jomouun"........"Ondoa shaka".Waliendelea na kasafari chao mpaka barabarani,Walisubiri muda mfupi tuu wakapata kausafiri/Bajaji.........

NDUGU MSOMAJI KATIKA MAISHA YAKO USIJE KUMRUHUSU SHETANI KUINGIA KWENYE HIMAYA YA NAFSI YAKO KWANI SHETANI ANA MBINU NYINGI ZA KUITEKA AKILI YA BINADAMU.MUNGU ANAKUPIMA IMANI KWA KUKULETEA MAJARIBU MAKUBWA SANA ENDAPO UKIWEZA KUYASHINDA BASI WEWE UTAUONA UFALME WA MUNGU LAKINI UKISHINDWA UTAUSIKIA UFALME WA MUNGU NA KUUSOMA KWENYE VITABU VYAKE.

Je mike ndio kashatekwa au naye anamchezea game Shania??....Usikose picha inayofuata