Wednesday 25 October 2017

Giggs asema anazitamani Everton na Leicester City

Kocha msaidizi wa zamani wa Manchester United Ryan Giggs amesema anatamani kuchukua mikoba ya makocha Ronald Koeman na Craig Shakespeare katika klabu za Everton na Leicester City.

Giggs ambaye alikuwa msaidizi wa Louis Van Gaal ndani ya Manchester United ameweka wazi nia yake hiyo wkaati akifanya mahoajiano na Sky Sports kuhusiana na uelekeo wake kwenye kufundisha soka.

“Hizi ni klabu zinazonivutia kuzifundisha kutoakana na aina yake ya uchezaji na zina wachezaji ambao wana viwango bora”, amesma Giggs

Hata hivyo Giggs amegoma kuweka wazi endapo atatuma maombi kwa uongozi wa timu hizo ili kumpatia nafasi hiyo ya kuongoza benchi la ufundi.

Leicester City ilimfuta kazi kocha Craig Shakespeare wiki iliyopita kabla ya jana Everton kumfuta kazi Ronald Koeman. Giggs amekuwa nje ya masuala ya ukocha kwa kazi ya juu tangu alipoondoka Manchester United mwaka 2016 baada ya mkuu wake Van Gaal kuondolewa.