Tuesday 24 October 2017

Kilichojiri Kesi ya Lulu Mahakamani leo. Mke wa Dk Slaa akosekana ushahidi (+Audio)

Shahidi wa pili upande wa utetezi ambaye ni mke wa Dk Slaa, Josephine Mushumbushi, na pia aliyekuwa mmoja wa madaktari wa marehemu Kanumba, ameshindwa kufika mahakamani Jumanne hii kwa ajili ya kutoa ushahidi wake kutokana na sababu zilizoelezwa kuwa yupo nje ya nchi na hakuweza kupatikana moja kwa moja.


Akiongea na waandishi wa habari baada ya kesi hiyo kuahirishwa, mtaalamu na mfuatiliaji wa kesi hiyo amesema, “Mwanzoni wakati anasomewa maelezo ya awali walisema
Lulu angekuwa na mashahidi watano, jana baada ya yeye kujitetea ikaonekana kama wanataka kufunga maelezo lakini wakasema kuna shahidi mmoja ambaye ni muhimu ambaye walikusudia kumuita.”
Video Player
00:06
01:30
“Josephine Mushumbush, huyu ni mke wa Dkt. Slaa, lakini kwa bahati mbaya hayupo nchini na juhudi za kumpata zimekuwa ngumu, mawasiliano yamekuwa magumu. Kwa hiyo wakawa wameomba maelekezo yake aliyoyaandikisha polisi yaweze kupokelewa mahakamani hata bila ya yeye kuwepo. Hayo ndio yalikuwa yanasikilizwa leo kama yapokelewe au hapana, hili pingamizi la kupokelewa likapingwa na jaji upande wa serikali kwamba huyu wakili siyo competent kuanza kuyatoa haya kwa hiyo siyo custodion wa haya maelezo wala sio yeye aliyeyatoa,” ameendelea.

Ameongeza kwa kusema, “Kwa hiyo akasema yupo mtu ambaye ana mamlaka na anaweza akayatoa lakini siyo wakili halafu akageuka kama shahidi, maelekezo ya jaji ni kwamba maelezo haya yatatolewa mahakamani na askari polisi Detective sergeant Nengea ndio aliyerekodi anaweza kuyatoa mahakamani. Kwa hiyo Mahakama imeelekeza kesho yeye ndio aje ayatoe kesho shahuri litakapoendelea na imeomba samancy ya kuja kuyatoa haya.”