Tuesday 24 October 2017

Bei ya korosho yazidi kunona. Lindi

Bei ya korosho yazidi kunona.Na.Ahmad
IKIWA ni mnada wake wa kwanza kufanyika katika msimu wa 2017/2018,chama kikuu cha ushirika cha RUNALI mkoani Lindi, jana kilifanikiwa kuuza korosho kwa bei ya juu kuliko bei za juzi zilizonunuliwa zao hilo katika chama kikuu cha Lindi Mwambo.

Akizungumza kutoka Mandawa,wilaya ya Ruangwa ambako mnada huo ulifanyika,Ofisa ushirika katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi,Robert Nsunza,alisema korosho ghafi zenye ubora wa daraja la kwanza, katika mnada huo bei ya juu ilikuwa shilingi 3,875 /- kwa kila kilomoja.Amapo bei ya chini ilikuwa shilingi 8,660/-.

Nsunza alisema bei hizo nitofauti na mnada uliofanyika katika chama kikuu cha Lindi Mwambao.Ambapo bei ya juu ya kila kilo moja ilinunuliwa kwa shilingi 3,850/-.Huku bei ya chini ya zao hilo linalozalishwa kwa wingi katika mikoa ya Lindi na Mtwara ilikuwa shilingi 3,810/-.

Ofisa ushirika huyo alisema katika mnada huo jumla ya barua za maombi za wanunuzi zilizopokelewa zilikuwa 32.Ambapo kampuni tatu tu kati ya hizo ndizo zlizofanikiwa kuteuliwa kununua korosho zote.

"Korosho zote zilikuwa tani 2717 na kilo 224,bei ya juu ilikuwa shilingi 3,875/-.Bei ya chini shilingi 3,660/-,nidhahiri bei imeongezeka ukilinganisha bei za jana(juzi),"alisema Nsunza.

Ofisa huyo mwenye dhamana ya ushirika mkoani humu alizitaja kampuni zilizoshinda zabuni kuwa ni Kasuga General,Maviga E A Ltd na RCN tz Ltd.

Mbali na kueleza hayo,ofisa ushirika huyo alitoa wito kwa wakulima kuchagua vizuri korosho na kuziweka kwenye madaraja yanayositahili ili ziweze kuendelea kununuliwa kwa bei nzuri.Huku akiwakumbusha kufungua akaunti ili malipo yao yapitie kwenye akanti za benki watakazofungua.

Nsunza aliwatoa hofu kuwa serikali imejipanga vizuri kuhakikisha hakuna uchelewashaji wa malipo unaoweza kutokea kutokana na sababu zisizo na msingi.

Ununuzi wa zao hilo katika msimu wa 2017/2018 ulianza rasmi tarehe Mosi,mwezi huu.Ambapo kwa mujibu wa bei elekezi iliyotangazwa na serikali kupitia bodi ya korosho ( CBT) bei ya kilo moja ya korosho ghafi za daraja la kwanza ni shilingi 1,450/-MWISHO.