Friday 30 June 2017

Mcheza tenisi Venus Williams ahusishwa na mauaji

Afisa mmoja wa kituo cha polisi cha Palm Beach Gardens mjini Florida amesema nyota wa mchezo wa tenisi Venus Williams amehusika katika ajali ya barabarani iliyosababisha kifo cha mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 78.


Mcheza tenisi,Venus Williams 

USAJILI: Tetesi za usajili barani ulaya

Tetesi za usajili barani ulaya klabu ya Valencia yaafiki kumpeleka kiungo wake Enzo Perez, katika timu ya River Plate na hatimaye mchezaji Jermain Defoe (34) katua Bournemouth kwa mkataba wa miaka 3.


Mchezaji wa Valencia ,Enzo Perez

Y Tony azidi kupagawa na Kajala

Msanii wa Bongo Fleva, Y Tony ameendelea kuweka hisia zake wazi kwa mrembo kutoka Bongo Movie, Kajala huku akikanusha tetesi za kuwa na mtoto.


Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake ‘Safina’, amesema uwepo wa Kajala ni moja ya sababu za kumfanya yeye kuendelea kujitahidi kufanya muziki mzuri.

Makabila yanayokula Nyama za Binadamu

UKIHADITHIWA tu na mtu yeyote unaweza kusema ni hadithi ya kutungwa, lakini ukweli ni kwamba kuna watu huko kwenye visiwa vya Papua New Guinea ambavyo vimezungukwa na bahari inayoitwa Bismarck Sea wanakula binadamu wenzao.

Rais Magufuli Apeleka Kilio Kwa Mbunge Joshua Nassari

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joshua Nassari huenda bado hajaelewa nini kielikumba jimbo hilo baada ya Diwani wa Kata ya Muriet, Credo Kifukwe kujiuzulu wadhifa huo kwa kile alichosema kuwa anamuunga mkono Rais Dkt Magufuli.

Albamu ya Jay Z yatua sokoni

Albamu ya rapper Jay Z imeanza kupatikana leo ikiwa zimepita siku kadhaa tangu alipoutambulisha ulimwengu kuhusu ujio wa album yake hiyo ya 13 iitwayo, 4:44.


Inadaiwa kuwa kati ya ngoma 10 ambazo zinapatikana katika albamu hiyo zimetayarishwa na producer No I.D.

Mjue Mgunduzi wa BUNDUKI MAARUFU IITWAYO AK 47

Luteni Jenerali Mikhail Timofeyevich Kalashnikov wa Urusi ndiye mgunduzi wa silaha maarufu sana katika uwanja wa mapambano duniani kote iitwayo AK 47. Ni bunduki iliyobuniwa na kutengenezwa na kamanda huyu wa Jeshi Jekundu (Red Army) la Muungano wa Kisovieti wa Urusi (USSR) wakati huo.

Huyu ndiye mchezaji ghali zaidi Everto FC inayodhaminiwa na SportPesa

Imechukua zaidi ya miaka 10 kwa klabu ya Everton FC, kufikia mafanikio ya mchezaji wao Duncan Ferguson raia wa Scotland aliyetokea klabu ya Rangers mwaka 1993 kwa dau lililoweka historia kwa wakati huo ndani ya Everton la uhamisho wa pauni milioni 4.

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa yaScotland na klabu ya Everton, Duncan Ferguson 

Taifa Stars Yatinga Robofainali COSAFA

Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imefuzu hatua ya robo fainali ya mashindano ya michuano ya COSAFA inayo endelea huko nchini Afrika Kusini baada ya kutoka sare ya goli moja kwa moja dhidi ya Mauritius.

Uchapa kazi wa RC Anna Mghwira wamgusa Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mama Anna Mghwira kwa kudhibiti usafirishaji wa mahindi nje ya nchi ambayo yalikamatwa kwenye Malori zaidi ya 103 yakisafirishwa nchi jirani.


Waziri Majaliwa ametoa pongezi hizo jana katika kipindi cha maswali kwa Waziri mkuu maarufu kama maswali ya Papo kwa Papo.

Kutana na Jambazi Aliyeiba Fedha Kwenye Banks 50 Kwa Ustadi wa Hali ya Juu zaidi Duniani

Mwaka 2021 ulimwengu utashuhudia mmarekani aliyefanikiwa zaidi kutekeleza matukio ya ujambazi akitoka gerezani baada ya kutumikia kifungo cha miaka 17 baada ya kufanikiwa kuishawishi serikali na mahakama kupunguza kifungo chake kutoka miaka mia moja kumi na tano (115) mpaka miaka hiyo 17.

Chagua Kufanya Mambo Haya, Ili Yakupe Mafanikio Makubwa

Siku zote maisha ya binadamu yanaongozwa na uchaguzi tunaoufanya kila siku. Uchaguzi huo ndio unatufanya tuwe na maisha haya au yale. Kama uchaguzi unaoufanya ni mbovu kila siku, basi ni wazi na maisha yatakuwa mabovu vilevile. Na kama uchaguzi wako ni mzuri,

Dawa Mpya ya UKIMWI Yaanza Kutumika Kenya

Hatimaye Kenya imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuanza kutumia vidonge vya ugonjwa wa Ukimwi ambavyo vinaweza kuboresha afya na kurefusha maisha ya maelfu ya watu wanaosumbuliwa na magonjwa nyemelezi na ambayo hayakubali tiba nyingine.

Thursday 29 June 2017

EMMANUEL Mbasha Amkana ‘Mchumba’ke’

BAADA ya kudaiwa kumvisha pete ya uchumba mshiriki wa Miss Tanzania 2008, Jacqueline Chuwa ‘Jack’, Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha amemkana akidai hamfahamu mlimbwende huyo.

WEMA Sepetu Ajipanga Kutii Wito wa Shehe Mkuu

MALKIA wa Bongo Muvi, Wema Isaac Sepetu anajipanga kutii wito wa Shehe Mkuu wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum wa kumtaka kufika ofisini kwake kwa ajili ya kisomo maalum ili kumuepusha na mabalaa ambayo yamekuwa yakimuandama.

Kampuni ya Google yapigwa faini ya dola bilioni 2.7

Google imepigwa faini ya dola bilioni 2.7 na tume ya ulaya baada ya tume hiyo kudai kuwa kampuni hiyo ilikuwa imekiuka mamlaka yake ya kuweka matangazo yake binafasi kuwa ya kwanza.

Faini hiyo ndiyo kubwa zaidi iliyotolewa na tume ya ulaya hadi leo, kwa kampuni ambayo imelaumiwa kwa kukiuka sheria za biashara.

Anachojutia Huddah katika maisha yake

Kila mtu ana mabaya na mazuri yake katika maisha. Mrembo Huddah Monroe ambaye anafahamka sana kwenye mitandao ya kijamii ameonyesha kujutia kuingia katika mahusiano.



Wolper apata mrithi wa Harmonize?

Msanii wa filamu Bongo, Jackline Wolper huwenda amepata mrithi wa aliyekuwa mpenzi wake Harmonize.


Wolper baada ya kuachana na msanii huyo wa muziki kutoka lebo ya WCB amekuwa akipost katika mtandao wa kijamii wa Instagram juu ya na kuonesha kuwa she is move on.