Thursday 29 June 2017

Witnes adai kufanya mapenzi kunapunguza unene

Msanii wa Bongo Fleva, Witnes a.k.a Kibonge Mwepesi amesema kufanya mapenzi kunapunguza unene.


Muimbaji huyo wa zamani wa kundi la Wakilisha ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa kuna vitu vingi ambavyo hupelekea mtu kupungua unene lakini ufanyaji wa mapenzi walau mara tatu kwa wiki kunasaidia.

“Lakini unatakiwa kujua kwa wiki unafanya mapenzi mara ngapi. Ni vema si chini ya mara tatu kwa hiyo kwa mwezi mara 12 lakini ukiweza kuzidisha zaidi ni fresh,” amesema Witnes.