Thursday 29 June 2017

Baraka The Prince aeleza sababu ya wimbo wake ‘Acha Niende’ kufeli

Muimbaji wa muziki Baraka The Prince amedai tatizo la nyimbo nyingi za wasanii kutofanya vizuri hivi karibuni ukiwemo wimbo wake mpya ‘Acha Niende’, linatokana na hali ya muziki kubadilika hivi karibuni huku akidai siasa ni moja kati ya vitu vilivyosababisha tatizo hilo.

Muimbaji huyo amedai amegundua wimbo wake mpya ‘Acha Niende’ umeshindwa kufikia malengo kutoka na kipindi kibaya cha mpito ambacho wanakutana nacho wasanii Wendi.

“Hali ni ngumu kweli kwa wasanii, nyimbo nyingi ambazo zimetoka hivi karibuni zimeshindwa kufanya vizuri kusema kweli hata wimbo wangu haujafikia kwenye malengo ambayo nilijiwekea wakati natoa au hata nikilinganisha na nyimbo zangu zilizopita,” Baraka alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.

CEO huyo wa Pana Music amedai moja kati ya sababu zilizosababisha hali hiyo kutokea ni matukio ya kisisa ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara.