Friday 16 June 2017

Simba SC yavuta mwingine kutoka Mtibwa Sugar

Kiungo wa Klabu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro, Ally Shomari ni rasmi mali ya Simba SC hii ni baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili.

Ally Shomari akisaini kandarasi ya miaka miwili kuichezea klabu ya Simba.

Kiungo huyo mwenye uwezo wa kucheza namba 2, 7, 6, 8, 10 na 11 anaonekana ndiye atachukua nafasi ya Ibrahim Ajibu anayekwenda Yanga.

Mchezaji huyo ambaye ametambulishwa rasmi na makamu wa Rais wa Simba Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, amesaini na Simba mkataba wa miaka miwili.

Bila shaka mashabiki na wapenzi wa klabu ya Simba wanafuraha kubwa kuona timu yao ipo bize katika usajili na wengi wanatarajia Simba mpya na yenye makali msimu ujao. Lakini je, Wachezaji hao waliosajiliwa na simba wataisaidia kufika inakotaka? Tusubiri hadi mwisho wa msimu.