Thursday 29 June 2017

Picha: Rayvanny anavyokatisha mitaani na tuzo ya BET

Kushinda tuzo ya BET ni ndoto ya wasanii wengi duniani – Kwa rayvanny ni kitu ambacho tayari atakuwa akikikumbuka katika maisha yake yote ya muziki na hata kuja kuwahadithia wajukuu zake hapo baadae.


Msanii huyo ameonekana akiwa yupo karibu na tuzo yake ya BET aliyoshinda Ijumaa iliyopita mjini Los Angeles katika kipengele cha Internationa Views Choice, katika kila mtaa anaokatisha ikiwa ni ishara kuwa hiko ni moja ya kitu muhimu baada ya mwanae Jaydan.


Ray alinyakuwa tuzo hiyo kwa kuwabwaga wasanii wengine kama Dave (Uingereza), Amanda Black (Afrika Kusini), Changmo (Korea Kusini), Daniel Caesar, Remi na Skip Marley (Jamica).

Hitmaker huyo wa Zezeta anatarajiwa kutua leo (Jumatano) majira ya saa nane mchana katika uwanja wa ndege wa JK. Nyerere akitokea Marekani kwenye tuzo hizo.