Thursday 29 June 2017

Rais Magufuli awapongeza wajumbe wa kamati za Makinikia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amekutana na wajumbe wa kamati zilizofanya uchunguzi wa mchanga wa madini huku serikali ikiahidi kuzifanyia kazi taarifa zilizotolewa na kamati hizo.


Rais Magufuli ameyaeleza hayo kupitia taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu leo.

“Timu hiyo imefanya kazi nzuri na yenye maslahi makubwa kwa Taifa na kwamba Serikali itahakikisha inafanyia kazi taarifa zilizotolewa na kamati hizo,” imeeleza taarifa hiyo.

Kamati hizo ziliyoongozwa na Profesa Abdulkarim Mruma na ya pili iliongozwa na Profesa Nehemia Osoro.