Thursday 29 June 2017

Kwangu ‘kiki’ zinakuja zenyewe, sitengenezi – Ben Pol

Msanii wa muziki wa R&B Ben Pol amefunguka kwa kukanusha kwamba siku hizi muziki wake anauendesha kwa kutegema kiki na sio kama zamani alivyokuwa anafanya.


Muimbaji huyo amedai kiki nyingi ambazo baadhi ya watu wanadhani anazitengeneza zinakuja zenyewe.

“Sio kweli kwamba nimekuwa msanii wakiki, siku hizi naweza kupigiwa simu sijui chochote nikaulizwa jambo ambalo hata silijui na kusababisha watu kudhani mimi natengeneza mazingira. Mambo mengi ambayo mmekuwa mkiyasikia yanatokea yenyewe sio kwa kupangwa na mtu,” Ben Pol alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.

Ben ambaye anafanya vizuri na wimbo wake uitwao, Tatu, amehusishwa kuwa miongoni mwa wasanii wanaotafuta kiki kwaajili ya muziki wake baada ya matukio kadhaa kutokea hivi karibuni likiwemo la mchekeshaji wa Timamu Media, Ebitoke ambaye alitangaza hadhani kwamba anampenda muimbaji huyo.