Thursday 31 August 2017

Chid Benz: Ni kweli nilikamatwa ila si madawa

Rapa kutoka kundi la LaFamila, Chid Benz ametoa ufafanuzi wa kukamatwa kwake siku ya Agosti 12 mwaka huu baada ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroine.


Chid amekanusha vikali tuhuma hizo kupitia E-Newz ya EATV na kusema kuwa stori hizo zinatengenezwa na washindani wake ili kumharibia kimuziki.

Jinsi Ya Kutoka Katika Kifungo Cha Umaskini

Kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine kuna changamoto ambazo zinamkabili kuweza kupata mafanikio zaidi. Na hizo changamoto ndizo ambazo tunaziita kifungo cha umaskini, kwani kifungo hicho kinampelekea mtu huyohuyo kutokuwa na uhuru wa kipato, muda na kifikra.

SEHEMU YA 03: DADA VUA


Huku upande wa pili Bright(Sule) na Hellen(Helena) Waliagana kila mmoja akimgeukia mwenzake,Helena alimtazama kwa umakini sana huyu kijana na kugundua ya kuwa Sule alikuwa na mawazo sana.Helena aliamua kusimama na kumtazama.Helena alishusha ndoo yake kisha akaamua kumfuata huku akaita "BRIGHT!!! WEE BRIGHT!!!!"

ilipendwa yaishusha Seduce Me katika trending

Vita ya trending katika mtandao wa YouTube haimuachi mtu salama!


Kwa mujibu wa mtandao wa YouTube unaotumika kuwekwa video mbalimbali za muziki, umeonyesha kuwa ngoma ya ‘Zilipendwa’ ya WCB imeshika namba moja katika trending huku ikifuatiwa na ‘Seduce Me’ ya Alikiba.

Music: Barnaba – Mapenzi Jeneza


Muimbaji Barnaba Classic baada ya kufanya vizuri na wimbo wake ‘Lover Boy’, ameachia wimbo wake mpya uitwao ‘Mapenzi Jeneza’. Wimbo huo umeandaliwa na Producer Ema the Boy.

Mghana apewa viatu vya Okwi

KOCHA MKUU WA SIMBA MCAMEROON, JOSEPH OMOG.
KOCHA Mkuu wa Simba Mcameroon, Joseph Omog, amesema anatarajia kumtumia mshambuliaji wake, Mghana Nicholas Gyan "kuvaa viatu" vya Emmanuel Okwi katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC itakayopigwa Septemba 6, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kimenuka: Chadema yatangaza mgogoro na serikali

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza mgogoro na mkuu wa wilaya ya Momba, Juma Irando kwa kuagiza jeshi la polisi wilayani humo kumuweka ndani kwa saa 48 mbunge wa Jimbo la Tunduma, Frank Mwakajoka kwa madai ya uchochezi.

USHAURI; Jinsi Ya Kuondokana Na Tabia Ya Matumizi Mabovu Ya Fedha Na Kuweza Kujiwekea Akiba

Mambo yote kuhusu fedha yanaanzia kwenye misingi miwili muhimu kuhusu fedha. Misingi hii ni mapato na matumizi. Kila kitu kuhusu fedha, iwe ni kuishiwa, kuwa masikini, kuwa tajiri na hata kuwa na akiba na kuwekeza kutaanza na misingi hiyo miwili, mapato na matumizi. Matatizo yote ya kifedha na hata mafanikio yote ya kifedha yanaanza na

Kuwa Tajiri kwa Mtaji wa Laki 3 tu, Kupitia Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji

LEO TUANGALIE MCHANGANUO WA TSHS 300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MRADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.

Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu 300 au na zaidi kama unataka.
Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.

Emirates yafanya Uteuzi wa Meneja Mkuu Mpya kwa Tanzania

Emirates imetangaza uteuzi wa Mheshimiwa Rashed Alfajeer kuwa meneja mkuu mpya nchini Tanzania.

Bwana Alfajeer, kutoka katika nchi za kitaifa wa Falme za Kiarabu, atakuwa na jukumu la kusimamia shughuli zote za emirates za kibiashara, wateja na mizigo kwenye soko.

Simba sasa kumburuza Buswita mahakamani

 
MKUU WA IDARA YA HABARI NA MAWASILIANO WA SIMBA, HAJI MANARA.

LICHA ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kumfungia kiungo wa Mbao FC, Pius Buswita, kutocheza soka kwa kipindi cha mwaka mmoja kutokana na kusaini kuzichezea klabu mbili tofauti, Simba na Yanga, sasa ataburuzwa mahakamani, imeelezwa.

Niyonzima afunguka uhusiano wake na Kabula

Kabla ya Jini Kabula kuwa katika matatizo aliwahi kunukuliwa akisema aliwahi kuwa mapenzini na staa wa soka wa Simba SC, Haruna Niyonzima na kuzua mzozo kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa Niyonzima kwenye ndoa hivyo kumsababishia matatizo ndani ya familia yake.

Wednesday 30 August 2017

Mbunge wa Tunduma atakiwa kukamatwa

Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Momba mkoani Songwe imeagiza kukamatwa mara moja kwa Mbunge wa Jimbo la Tunduma kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh.Frank Mwakajoka kwa tuhuma za kuwadhihaki wateule wa Rais.

Msafara wa DC washambuliwa na watu wasiojulikana

Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheluka 
Karagwe. Msafara wa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheluka uliokuwa katika operesheni ya kuwaondoa watu wanaodaiwa kuvamia maeneo ya wafugaji katika Kijiji cha Kashanda, Kata ya Nyakahanga, umeshambuliwa na watu wasiojulikana.

Halima Mdee awafungukia Polisi

 
Mbunge wa Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Halima Mdee amefunguka na kusikitishwa na jeshi la polisi kushindwa kuwakamata matapeli ambao wamekuwa wakitapeli wananchi kwenye mitandao kupitia jina lake.

Manara atema nyongo

Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara
Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amefunguka kwa kuwatupia lawama Bodi ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwa wanachokifanya siyo sawa wanabidi wabadilike.

Hii ndio sababu ya duka la Jux kuvunjwa

Jux ambaye ni mmiliki wa duka linalo uza nguo za 'brand' yake ya 'African Boy', ametoa sababu iliyofanywa duka hilo lipitiwe na bomoa bomoa, katika eneo la Sinza jijini Dar es salaam.

Rapa wa Kenya amvulia kofia Jux

Rapa Nyashinski kutoka nchini Kenya ambaye sasa anafanya vyema na ngoma yake 'Aminia' amefunguka na kunyoosha mikono kwa msanii wa bongo fleva Jux African Boy ambaye sasa anafanya vyema na ngoma yake mpya 'Utaniua'.

Trump atoa agizo hili

Rais wa Marekani Donald Trump ameondoa marufuku iliowekwa na Obama kuhusu kuwapatia maafisa wa polisi vifaa vya kijeshi.

Hii ndio Siri ya Jux kupenda mastaa

Mkali wa muziki wa Rnb Juma Jux ambaye anasumbua na ngoma ya 'Utaniua' amefunguka na kusema kuwa ingawa kwa sasa yupo Single baada ya kuachana na msanii Vanessa Mdee, kamwe hafikirii kuwa na mwanamke ambaye ni tegemezi na hana cha kupoteza.

Njia za Kujikinga na Magonjwa ya Moyo

Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu (cardiovascular diseases) yamekuwa yakiongezeka kwa kasi katika nchi za Afrika kinyume miaka ya nyuma. Kati ya sababu mojawapo ni mabadiliko katika mitindo ya maisha na lishe. Watu wengi hawana mazoezi na wanakula vyakula vyenye nishati nyingi (energy dense diet) kuliko vyenye virutubisho kwa wingi (nutrient dense diet), na hili linachangia sana kuongezeka kwa kasi kwa magonjwa haya.

Tuesday 29 August 2017

Zifahamu dalili za ugonjwa wa saratani

Saratani ni ugonjwa unaotokana na kushindwa kudhibiti ukuaji wa chembe mwili. Saratani hudhuru mwili kwa chembe zilizoathirika zinapogawanyika bila utaratibu unaofaa na kuweka mikusanyiko ya uvimbe ya chembe hai.

Sababu ilioyomuondoa Baraka Rockstar ni hii

Baada ya muda mrefu wa maswali juu ya sababu iliyomfanya msanii Baraka The Prince kutoka kwenye lebo kubwa ya muziki ambayo ilimsaini ya Rockstar4000, hatimaye mmoja wa mabosi wa lebo hiyo msanii Alikiba aweka wazi kila kitu.

Zijue Mbinu za kuondiokana na Tatizo la Kunuka Mdomo

Tatizo la kunuka mdomo limekuwa ni kikwazo kikubwa kwa watu wengi. Halitosis kitaalum ni ile hali ya kuwa na harufu mbaya mdomoni, hali hii inaweza kuathiri maisha ya mtu kimahusiano si kwa mpenzi tu bali marafiki na jamii kwa ujumla.