Tuesday 29 August 2017

Afrika ya Kati hali si shwari

Kikundi kimoja cha kutoa misaada ya kimataifa kinasema hakiwezi kufikia maeneo mawili ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kutokana na eneo hilo kutwaliwa na Wanamgambo .

Kikundi hicho Mercy Corps kimeeleza kuwa watu wapatao elfu thelathini katika miji ya Niem na Yelewa haina msaada wowote. Katika kijiji kimoja, yatima wapatao laki moja na thelathini wanapata matunzo kwa familia za maeono hayo.

Karibu wafanyakazi mia mbili wafanyakazi wa kutoa misaada wameshambuliwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Inaarifiwa kuwa zaidi ya nusu ya watu katika Jamhuri hiyo wanategemea misaada ya kibi9naadamu ili kuishi.

Zaidi ya watu milioni moja wamepoteza makaazi yao na kuelekea kusikojulikana kutokana na mzozo ulioanza mnamo mwaka 2012.