Wednesday 30 August 2017

HADITHI; DADA VUA SEHEMU YA 2

TUNAKULETEA HADITHI MPYA KILA SIKU ASUBUHI USIKOSE Download App Hii Kupata Kwa Wakati>> https://play.google.com/store/apps/details…

πŸ‘™πŸ‘™πŸ‘™ DADA VUAπŸ‘™πŸ‘™πŸ‘™
PICHA NO:_2
Sule alinyanyua kibegi chake vizuri kisha akakiweka mgongoni na kuelekea Ngare.Kweli aliondoka akipitia barabara ya msitu wa Momela/Arusha National Park.Akiwa anaanza kuingia katika pori la msitu alihisi kitu kinatokea mbele yake maana alisikia mchakacho,Basi Sule aliamua kujibanza kwenye shina la mti ili kama ni kitu cha hatari aweze kukabiliana nacho
SHARE NA MARAFIKI KWENYE GROUP ZA WHATSAPP WAPATE UHONDO NAO
Sule akiwa na mawazo tele juu ya kile kilichotokea nyumbani alitembea huku akiwa na mawazo sana.Njia nzima alipiga miluzi akiimba nyimbo mbali mbali za huzuni,Ilikuwa ni safari ambayo Sule hatokaa aisahau.
Kutokana na mchakacho ule na kwa kuwa alikuwa hajajiandaa vyema aliamua kujificha ili kama ni mnyama wa hatari apite tuu asije kudhurika.Lakini wakati anayatoa macho pale alipousikia mchakacho aliona kitu tofauti na alichodhania.Alikuwa ni msichana mrembo,mwembamba na mweupe akiwa amebeba ndoo ya maji.Sule alimtazama kisha akajisemea"Kumbe mtu unaweza ukafa na presha bure kwa woga sasa kipi kilichonifanya niogope kiasi hichi heheee".Sule alijicheka kwani aliona kama vile limnyama likubwa linatokea kumbe ni bonge la toto.Lakini Sule alianza kujiuliza...."Sasa inakuaje huyu msichana anakuja kuteka maji mbali kiasi hiki halafu mavazi aliyoyavaa na mazingira haya akikutana na vidume vyenye njaa njaa si vinamfaidi!?".

Sule alianza kumtafakari yule binti kwani mavazi aliyoyavaa na mazingira aliyopo ni hatari kwake.Basi Sule alitoka na kuendelea na safari yake,Kilichomshangaza zaidi Sule ni kwamba binti yule alizidi kuingia kule kule msituni.Aliwaza"Sasa huyu anaenda wapi huku inamaana huku ndani ya msitu kuna nyumba!? mmmh!! Anyway kwa sababu sijapita huku siku nyingi labda kuna makazi ya watu huku .Mara ghafla yule dada alisimama kisha akaishusha ile ndoo na kuiweka chini wakati huo dada huyo hakumuona kabisa Sule,Dada aliishusha ndoo na kuingia kichakani haraka haraka.Sule alisimama naye akajifanya anakojoa,Mara akasikia sauti ya mtiririko wa mkojo......."CHROOOOOOO!!!"......Sule aliguna tuu "Mhhhh!! kaniona nini mbona kama kananitega".
Dada yule kwa kuwa hakujua kuwa kuna mtu nyuma yake alitoka huku akilazimishia kukivaa kile kikaptula cha jinsi.Kilikuwa kimembana sana kiasi kwamba kina mlazimu kutumia nguvu sana pindi avaapo.Sule alimtazama yule binti anavyohaingaika,Ndipo macho ya yule binti yalipo kutana na kidume handsome.Sule alikodolea macho pale kwenye kalio kwani kaptula iligoma kabisa kufika kunako kiuno.Basi yule binti ilibidi arudi nyuma ili aweze kumalizia kuvaa.Sule alianza kuingiwa na tamaa akajikuta anamwambia" Sasa waogopa nini bibie!!?".Binti kwa aibu alijikuta amenyamaza kimya bila hata kutoa neno,Binti yule alijitokeza kisha akawa anajitwika ile ndoo,Muda huo tayar Sule alikuwa miguuni mwa binti.Sule alijikuta anamsaidia binti yule kumtwisha ile ndoo"Pole sana dada yangu"......Binti alimjibu"Asante!".....Sule hakuishiwa na maneno...."Mbona unanijibu shortcut sana au nimekosea kukusaidia"...."Mmmmmmh!! hayo umesema wewe kaka mimi aaaka!!".
Sule hakutaka kupitwa na toto la kimeru alijikuta anamwambia"Basi fanya hivi shusha hiyo ndoo nikusaidie,kwani kwenu ni mbali!!?"......"Hapana sio mbali ni hapo chini"......Binti aliongea huku akimuonyeshea kwa kidole.Basi Sule aliyapanga maneno mtoto akajikuta anakubali kusaidiwa ile ndoo.Sule alimuuliza"Mbona hatufiki???"......"Kama umechoka nipe tuu mi ntamalizia".....Sule alijibu kiustadi kabisa"Simaanishi kuwa nimechoka bali nakuonea huruma kwani unachota maji mbali sana"......"Tumeshazoea kwani wewe unaitwa nani na unakwenda wapi"........Sule aliwaza kabla hajatoa jibu kisha akajibu"Naitwa Bright na nimeamua tuu kunyoosha nyoosha miguu huku nikivinjari madhari ya msitu huu"......."Waoooo jina zuri sana sasa huku kuvinjari gani porini huogopi wanyama??"Binti aliuliza huku akiishika ndoo upande wa pili wakisaidiana na Sule......"Ntaogopa vipi mi wa kiume wewe!!! kwanza siku hizi hakuna hata hao wanyama na wewe unaitwa nani??" Sule aliongea kwa mbwembwe kwani hata jina alimpa la uongo......Dada huyu jina lake kamili anaitwa HELENA lakini kwa kuwa Mshkaji kataja jina lenye swaga naye alimjibu"Call me Maadam Hellen".
Kila mmoja alimfahamu mwenzake kisha helena akamwambia mwenzake Sule"Bright kwetu paaale tumeshafika"...."Hellen why mnachota maji mbali hivi ina maana kuna shida yamaji sana!!!?....."Sio mbali bhaana sema tuu hujazoea".Basi Sule alitaka kumuaga Helena kwani si vyema kwenda naye mpaka nyumbani"Basi mi nikuache niendelee na SAFARI yangu tutaonana mungu akipenda".Waliagana pale lakini Helena alionyesha sura ya huzuni kama vile alitaka kuendelea kumjua mtu huyu"Haya kaka yangu BRIGHT mungu akutangulie Siku ukipita njia hii usisite kuja nyumbani.
HUKU NYUMBANI KWA KINA SULE
Uliibuka mzozo mkubwa sana mara baada ya Sule kuondoka.Baadhi ya wadogo zake Sule hawakupenda kabisa kitendo walichokifanya wazazi wao kwani kutokumpa Sule haki yake kama kaka mkubwa wa familia hakikuwa kizuri.Wadogo zake Sule hawakujua kiundani kusudi la wazazi wao kufanya hivyo.Wakati wanaendelea na mzozo mama alitoka akiwa ana hasira sana.Basi mama aliimuita mumewe kwa sauti kali"Mume wangu unafikiria nini kuhusu hili mbona umekaa kimya!!?"......."Sikia mama Sule,Mimi kabla hata Sule hajawaza kufanya chochote tayari nilishawasiliana na mtaalam hivyo mambo yataenda sawia".Mzee alirudi mpaka sebuleni kisha akaanza kuwatuliza watoto wake ili wasije farakana.
Huku upande wa pili Bright(Sule) na Hellen(Helena) Waliagana kila mmoja akimgeukia mwenzake,Helena alimtazama kwa umakini sana huyu kijana na kugundua ya kuwa Sule alikuwa na mawazo sana.Helena aliamua kusimama na kumtazama.Helena alishusha ndoo yake kisha akaamua kumfuata huku akaita "BRIGHT!!! WEE BRIGHT!!!!"........... usikose inayofuata maana picha ndo kwanza linaanza.kule whatsapp zipo story tatu tofauti jiunge na sisi kwa sh 3000 tuu.
usiache kudondosha like kwani bila like mimi sipati mizuka yakuleta vitu adimu.
ALIKA RAFIKI ZAKO KWA KUSHARE ILI NAO WAPATE UHONDO HUU.