Thursday 31 August 2017

SEHEMU YA 03: DADA VUA


Huku upande wa pili Bright(Sule) na Hellen(Helena) Waliagana kila mmoja akimgeukia mwenzake,Helena alimtazama kwa umakini sana huyu kijana na kugundua ya kuwa Sule alikuwa na mawazo sana.Helena aliamua kusimama na kumtazama.Helena alishusha ndoo yake kisha akaamua kumfuata huku akaita "BRIGHT!!! WEE BRIGHT!!!!"

Shuka nayo.........MKIWA WAVIVU KUSHARE NTAKUA MZEMBE KUPOST.DONDOSHA LIKE NA MAONI YAKO

Maadam hellen aliamua kumuita Bright,Bright alisimama kwanza kwa sekunde kadhaa lakini hakugeuka kumtazama Hellen.Hellen alimuita tena " Sasa si uje heee!!!",Kiukweli Sule alivyoachana na Helena alifika mbali sana kimawazo mpaka akajikuta chozi likimdondoka.Sasa baada ya helena kumuita hakugeuka kwa sababu angegundulika kuwa alikuwa analia,Alijifuta machozi haraka haraka kisha akageuka akiwa na tabasamu feki ili kumzuga binti yule mrembo.Hellen alipomtazama Sule aligundua kuwa kuna kitu kinamsibu"Wee Bright uko sawa kweli!!!?"........"Yaah mbona niko poa kwani vipi!!!?........"Huenda hauko vizur ila wanificha tuu,nimekuona mwendo wako yaani kama vile kuna kitu kinakuumiza kichwa? We nambie tuu naweza kukusaidia hata kimawazo eti!!".Sule alikaa kimya kwa sekunde kadhaa akitafakari kwani helena kampa swali ambalo kiukweli sule anahitaji ushauri.

Baada ya Helena kuona Sule kawa mzito kumuelezea kinachomsibu alijaribu kumbembeleza ili wafike hata nyumbani kabla hajaendelea na safari yake.Sule hakuwa na kipingamizi kwani hata anakoenda hana uhakika sana kama atafanikiwa kupata shughuli aliyoikusudia.Helena alijaribu kutumia maneno mazur ili kumuweka sawa huyu kijana Sule.Sule alimuuliza Helena"Sasa Hellen unaishi na nani hapo kwenu!!?"...... Helena alicheka"hehee!! mbona unajishuku sana usiogope Bright naishi na dada yangu pamoja na Shangazi"......."Sule alitamani kumjua kiundani zaidi lakini aliona kama atamchosha binti kwa maswali"mmmmmh!! haya lakiiiiini!!!?"....."Bright acha maswali ya uoga we twende?".Yalikuwa ni mazungumzo ambayo yalimshawishi kidume huyo kukubaliana na sweet manka HELLEN.

Wakati huo shangazi yake helena alikuwa kwenye banda la mifugo akiwahudumia wanyama wake kwani anapenda sana ufugaji.Shangazi alitupa macho kwa mbali alimuona Helena akiwa anakuja na mtu asiyemjua.Shangazi alimuita dada yake Helena"Weee Lucy!!!!".....Lucy alikuwa chumbani"Beee!!"....."Njoo uone huyu mwenzako zoa zoa sijui kabeba limtu gani!!?".Kiufupi shangazi huyu huwa hapendi sana wageni nyumbani kwake na hataki kabisa kina Helena wazoeane na mwanaume yoyote.Basi Lucy alivyosikia vile alitoka kisha akasimama nje na kutazama kule wanakotokea kina helena.Lucy alitazama kisha akarudi ndani haraka,Alivyofika akabadili nguo alizokuwa amezivaa alichukua kioo kisha akaanza kujaribu kama ataweza kucheza na lips ili kumtega huyu jamaa anayekuja na mdogo wake.Aliweka kila aina ya pozi kisha akajipuliza marashi na kutoka.

Wakati huo shangazi yake Helena aliacha hadi kuihudumia mifugo akabaki anamshangaa yule kijana,Alimtazama kwa hasira sana.

HUKU NYUMBA KWA KINA SULE

Baada ya Baba kukataa kabisa swala la kumgawia Sule mali wadogo zake waliamua kumpigia Simu sule ili arudi wakati wanaendelea kumbembeleza baba yao.Wedi alichukua simu kisha akawa anampigia kaka yake Sule,Simu ya Sule iliita lakini haikupokelewa.Wakati anaendelea kupiga mara Sudi alikuja huku akiongea "Simu yenyewe kaiacha chumbani kwake hii hapa".Kweli Sule aliiacha simu ndani na sijui kasahau au aliamua tuu.Wedi alizidi kupata hofu kwani anajua hasira za kaka yake"mhhhh! sasa kwanini kaacha simu!? usikute kaamua kufanya jambo lingine tofaouti" Yalikuwa ni mawazo ya Wedi.Wedi alimfuata mama yake na kumwambia"Mama unafikiria nini kuhusu swala la kaka Sule"......."Achana nae kwanza ana kiburi sana akiamua kurudi atarudi tuu".Wedi alitegemea mama atasaidia kumshawishi baba lakini alionekana kama hajali wala halimuumi swala la Sule kuondoka pale nyumbani.

HUKU KWA KINA HELENA

Lucy alitoka akiwa amejipodoa kweli kweli huku akizichezesha lips zake kama alivyokuwa akifanya zoezi kwenye kioo.Mara simu ya Shangazi iliita akawa anaongea huku akimtazama sana Sule,Sule hakujua ni kwanini Bibi huyu anamuangali huku anaongea na simu.Alimaliza kuongea na simu kisha akampokea Helena kwa maneno"We helena muda wote huo hayo maji ulienda kuyateka Usa au".

📝KWA WALE MLIOWAHI KUFIKA ARUSHA NADHANI MNAJUA USA IKO WAPI NA HUU MSITU WA MOMELA UKO WAPI📝

Basi Shangazi alimfokea bila kujali kuwa kuna ugeni amekuja nao,Helena hakujibu kitu shangazi alitupa tena dongo"Eheee na huyo ni nani!?? maana wewe hukawii kuniletea mijizi".......Lucy alidakia ....."Looooh!! shaangazi huogopi kutoa mineno hadi kwa wageni".Sule kuona vile alimwambia Helena"Aaaaamh!! hellen acha mi niende nisije kukugombanisha na shangazi yako"......"Bright usiogope huyu yukogo hivi anapenda sana kuongea".....Lucy naye alijichangamsha kwa Sule kama vile anamjua wakati ndio mara ya wa kwanza wanaonana "Kakaaa karibu usiogope mwaya karibu sana".Helena alitangulia ndani akiwa amebeba ndoo yake akawaacha Lucy na Sule nyuma.Lucy alikuwa na machachari sana mpaka Sule alishangaa" Mhhhhh!! huyu dada vipi kadata au!??" Mara Lucy akafunua kidogo nguo yake kwa pale kwenye nyonyo huku akimuonyesha Sule Vichuchu.......Usikose sehemu inayofuata maana hii ni zaidi ya movie.

usiache kudondosha like kwani bila like mimi sipati mizuka yakuleta vitu adimu.

ALIKA RAFIKI ZAKO KWA KUSHARE ILI NAO WAPATE UHONDO HUU.