Tuesday 29 August 2017

Tetemeko la ardhi laikumba Iran

Ripoti zinaonyesha kuwa tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 4.9 limeukumba mji wa Sharabian mashariki mwa Azerbaijan nchini Iran.

Kwa mujibu wa habari,uchunguzi uliofanywa na chuo kikuu cha Tahran nchini humo unaonyesha kuwa tetemeko hilo lilifikia kina cha kilomita sita.

Ni watu nane wameripotiwa kujeruhiwa katika tetemeko hilo.

Tetemeko hilo limesababisha baadhi ya nyumba kubomoka.

Jitihada za uokoaji zinaendelea.