Wednesday 30 August 2017

Mwanariadha David Torrence Wa Mbio Za Masafa Ya Wastani afariki Marekani

David Torrence wa Kwanza kushoto Mwanariadha wa Marekani
Mwanariadha wa mbio za masafa ya wastani kutoka Marekani David Torrence amepatikana amefariki katika kidimbwi cha kuogelea katika jimbo la Arizona akiwa na miaka 31.

Torrence alishinda fedha katika mbio za ubingwa wa dunia za kupokezana vijiti mwaka 2014 na alimaliza wa pili pia katika mbio za bara la Amerika mwaka 2015.
Alibadilisha uraia kutoka Marekani hadi Peru na akawakilisha taifa hilo lake jipya katika michezo ya Olimpiki ya Rio mwaka 2016.

"Wachunguzi wa jinai wamebaini kwamba hakuna dalili zozote dhahiri kwamba huenda aliuawa," taarifa ya polisi imesema.