Tuesday 29 August 2017

China yadai kupata ushindi dhidi ya India

China inasema kuwa India imeondoa majeshi yake kutoka maeneo wanayozozania katika mpaka kati ya nchi hizo mbili huko Himalaya, na kumaliza mtafaruku mkubwa uliokuwepo wiki iliyopita.

Wizara ya nchi za kigeni huko Beijing, inasema kuwa imefurahishwa kuwa "jeshi la India lililokuwa limevuka mpaka na kuingia kwenye ardhi ya China, limerejea ndani ya mpaka wao".

Wizara ya kigeni nchini India, imethibitisha kuwa wanajeshi wake, "kuondoka" huko Doklam baada ya makubaliano kati ya mataifa hayo mawili.

Mzozo kati ya mataifa hayo mawili yalianza katikati mwa mwezi Juni, pale India iliposema kuwa inapinga jitihada za China za kujaribu kuendelea kujenga barabara katika nyika iliyoko mpakani mwa mataifa hayo mawili.

Eneo hilo linajulikana kama Doklam huko India na Donglang nchini Uchina.

Taarifa hii inatukia wiki moja kabla ya Waziri mkuu wa India Narendra Modi kufanya ziara nchini China.

Eneo hilo tambarare, lililoko kwenye njia panda kati ya China na kaskazini mashariki mwa jimbo la Sikkim nchioni India na utawala wa Himalaya wa Bhutan, unazozaniwa na Beijing na Bhutan.

India inaunga mkono madai ya Bhutan.