Tuesday 29 August 2017

Manara: Niyonzima na John Bocco wapo fiti

Kiungo Haruna Niyonzima ameanza mazoezi na wenzake kujiandaa na michezo inayofuata ya Ligi Kuu Bara.

Niyonzima aliumia katika mechi ya kwanza ya ligi hiyo akiichezea Simba dhidi ya Ruvu Shooting.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amethibitisha Niyonzima kuanza mazoezi.

Pamoja na Niyonzima, Manara amesema, John Bocco naye ameanza kujifua na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mechi hizo zijazo.