Thursday 31 August 2017

Kumbe Chid Benzi Alikua Anatania Collabo na 2Pac? Hivi Ndivyo Alivyofunguka Kwa Mashabiki Zake

Rapa Chid Benz ambaye sasa anafanya poa na wimbo wake 'Muda' akiwa ameshirikiana na mkongwe Q Chillah amefunguka na kuwataka mashabiki wake kutosikiliza maneno ya watu na kudai wapinzani wake wamekuwa wakimuongelea vibaya kwa lengo la kumchafua


Chid Benz anasema muda mwingine kwenye maisha yake ya kila siku amekuwa ni mtu wa utani sana kiasi kwamba utani mwingine huwa hapendi hata ufike kwenye 'Camera' za watu kwa kudai unaweza kutafsiriwa ndivyo sivyo.

Rapa huyo ameibuka na kusema hayo ikiwa ni siku moja imepita toka alipotoa kauli kwamba anataka kumleta marehemu 2Pac nchini na kusema msanii huyo wa Marekani ni mzima na wala hajafa na kudai tayari wameshafanya naye wimbo.