Wednesday 30 August 2017

Halima Mdee awafungukia Polisi

 
Mbunge wa Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Halima Mdee amefunguka na kusikitishwa na jeshi la polisi kushindwa kuwakamata matapeli ambao wamekuwa wakitapeli wananchi kwenye mitandao kupitia jina lake.

Halima Mdee amesema kuwa ni muda mrefu alishatoa taarifa kwenye jeshi la polisi kuhusu watu hao wanaotumia jina lake kwenye mitandao ya kijamii na kujifanya kutoa mikopo yenye riba ndogo na kuwatapeli wananchi pesa zao.

"Wanaojitambulisha kutoa mkopo kwa jina langu ni matapeli, sihusiki nao !Nimetoa taarifa polisi inaonekana hawakamatiki" alisema Halima Mdee

Aidha watu hawa wanaojitambulisha kama Halima Mdee wanatumia mpaka jina la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika kufanya utapeli huu na kuwaumiza wananchi wa chini ambao wanashida na kutaka kujikwamua kimaisha kupitia mikopo hiyo na badala yake wanakwenda kuongeza matatizo kwani hata kidogo walichokuwa nacho pia hutapeliwa.

Mbali na Halima Mdee jina lake kutumika katika utapeli huu lakini pia viongozi wengine mbalimbali na watu maarufu wamekuwa wakitumiwa na watu hawa katika kuendelea kufanya utapeli huu, mfano jina la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Lakini pia Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe ameshawahi kulalamika juu ya utapeli huu unaofanya na watu hawa mitandaoni.