Thursday 31 August 2017

Rais Kagame amteuwa waziri mkuu mpya Rwanda

Rais Paul Kagame aumteuwa Edouard Nigirente katika wadhifa wa waziri mkuu wa Rwanda ambae alikuwa hafahamiki katika ulimwengu wa siasa

Rais wa Rwanda Paul Kagame amemteuwa Edouard Nigirente katika wadhifa wa waziri mkuu wa Rwanda Jumatano akiwa hatafahamiki katika ulimwengu wa siasa.

Waziri mkuu huyo mpya wa Rwanda amekula kiapo hapo Jana baada ya kuteuliwa na rais Paul Kagame.

Baraza la mawaziri nchini Rwanda linatarajiwa kupangwa katika siku za usoni.

Edouard Nigirente alikuwa mshauri katika osifi za Fuko la fedha mjini Washington.

Waziri mkuu huyo mpya alikuwa akifanya kazi katika ofisi za wizara ya fedha nchini Rwanda.