Wednesday 30 August 2017

Hii ndio Siri ya Jux kupenda mastaa

Mkali wa muziki wa Rnb Juma Jux ambaye anasumbua na ngoma ya 'Utaniua' amefunguka na kusema kuwa ingawa kwa sasa yupo Single baada ya kuachana na msanii Vanessa Mdee, kamwe hafikirii kuwa na mwanamke ambaye ni tegemezi na hana cha kupoteza.

Jux ameefunguka hayo leo kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio wakati alipokuwa akijibu swali la shabiki yake ambaye alihoji ni kitu gani ambacho anakikumbuka kutoka kwa mpenzi wake huyo na kusema kuwa ni mwanamke mchapakazi na mwenye kumfanya kila siku apige hatua.

"Vanessa namkumbuka kwa kila kitu kwa sababu nilimpenda na ninampenda sana. Kanifanya niweze ku focus kwenye mambo ya msingi kwa sababu na yeye ni mpambanaji. Niseme tuu siwezi kuwa na mwanamke ambaye sijui anafanya nini mjini. Mimi napenda mwanamke anayejituma" alisema Jux
Jux ameongeza "Kuna watu watasema oooh Jux anapenda sana mastaa labda ndiyo maana akawa na Jack au Vanessa.

Siyo kweli kwamba napenda mastaa sana lakini ukweli ni kwamba kwenye maisha yangu siwezi kuwa na mahusiano na mwanamke ambaye hana cha kupoteza, Naamanisha ambaye hana chochote ambacho anafanya, mfano Vanessa ana mashabiki so ni mtu ambaye alikuwa anayaheshimu mahusiano yetu kwani asingeweza kufanya ujinga ku dissapoint mashabiki zake. Kuna mwanamke anaweza kuamka asubuhi akabeba paspoti yako na usijue pa kumpata," .