Tuesday 29 August 2017

Chanzo cha majina ya mapacha wa Jay Z hiki hapa

Boss kutoka Roc Nation, Jay Z amefunguka chanzo cha majina ya watoto wake mapacha, Rumi na Sir waliozaliwa miezi miwili iliyopita.

Akiongea na mtandao wa Rap Radar, rapper huyo ambaye ni baba wa watoto watatu ameeleza kuwa majina ya watoto wake hao wawili yametokana na mashairi yanayopendwa na Ivy Blue.

“Rumi is our favorite poet, so it was for our daughter, Sir was like, man, come out the gate. He carries himself like that. He just came out, like, Sir,” amesema Jay.

Kwa sasa Jay Z anatamba na albamu yake ya 4:44, ambayo ilitinga sokoni Juni 30, 2017 ikiwa na ngoma takribani 10 huku mtoto wake wa kwanza Blue Ivy akihusika katika kufanya kolabo na baba yake.