Tuesday 29 August 2017

Liverpool yamsajili Naby Keita

Baada ya mvutano wa muda mrefu baina ya vilabu vya Liverpool na RB Leizpg hatimaye Liverpool wamefanikiwa kukubaliana na klabu hiyo kumnunua kiungo huyo.

Rb Leizpg walikataa ofa mbili ambapo moja inafahamika ilifikia kiasi cha £70m lakini sasa wamekubali kumtoa Keita kwenda Liverpool kwa ada ya £48m.

Hii ni rekodi mpya ya usajili katika klabu ya Liverpool baada ya ile ya Andy Caroll mwaka 2011 ambapo alisaini Liverpool kwa kiasi cha £35.

Lakini klabu hiyo ya Liverpool haitamtumia Keita hadi itakapofika mwezi July mwaka 2018, Leizpg wanataka kubaki na Keita katika msimu huu ambapo wapo katika michuano ya Champions League.

Huu ni usajili wa tatu kwa Liverpool kuufanya katika msimu huu wa ligi ambapo tayari walimnunua Mohamed Salah toka As Roma pamoja na Andrew Robertson toka Hull City.

Wakati Keita akielekea Liverpool klabu hiyo inatajwa kukaribia kukamilisha usajili wa kiungo Thomas Lemar ambapo inasemekana mabosi wanapambana ukamilike kabla ya tarehe ya mwisho ya usajili.

Monaco wanaonekana hawako tayari kumuachia Lemar aondoke lakini dau la £60m linaoneokana kuwavutia kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22.