Tuesday 29 August 2017

Sudan na Libya zimekubaliana kumaliza migogoro kati yao na kulinda mipaka yao.

Katika mkutano wa pamoja na waziri mkuu wa Libya Feyaz Mustafa al Sarraj katika mji mkuu wa Khartoum,rais wa Sudan Omer Al Bashir alionyesha mshikamano na serikali ya Libya.

Ziara ya rais wa Libya nchini Sudan imefuatia matatizo yaliyojitokeza mwezi Julai baada ya Libya kuiamuru Sudan kuufunga ubalozi wake mjini Kofra na kuwafukuza wanadiplomasia 12.

Kwa mujibu wa habari,rais wa Sudan amesema kuwa nchi yake haina ajenda yoyote na Libya bali inaitakia mafanikio nchi hiyo.

Rais huyo vilevile amesema hali mbaya ya Libya inaathiri usalama wa nchi ya Sudan.

Waziri Sarraj amesema kuwa nchi zote mbili zimejifunza mengi kutoka katika makosa yao na zinatumai kusonga mbele kimaendeleo.