Thursday 29 June 2017

Picha: Huyu ndio mpenzi mpya wa Rihanna!

Baada ya upweke wa muda mrefu bila ya mpenzi, Rihanna ameonekana kupata mpenzi mpya.


Mara ya mwisho mrembo huyo kuonekana akiwa katika hali ya mahusiano ni mwaka jana mwishoni alipodaiwa kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake Drake lakini walimwagana baada ya rapper huyo kuwa karibu na mwanamama Jennifer Lopezi.


Mrembo huyo ameonekana Jumatatu hii akila pata nchini Hispania [Posh Villa] akiwa na kidume ambaye ni sura mpya machoni mwa mashabiki wa mrembo huyo. Tazama picha nyingine zaidi hapa chini.