Wednesday 28 June 2017

Jinsi Coco Beach Ilivyofurika Juzi Jijini Dar es Salaam

Hivi ndivyo Ufukwe wa Coco (Coo Beach) ulivyofurika watu wa aina mbalimbali hapo jana jioni, katika kusherehekea sikukuu ya Iddi pili,Mabasi/Daladala kutoka kona kadhaa za jiji la Dar zilionekana zikishusha watu kwa wingi katika ufukwe huo ambao ulisheheni pia vyakula vya kila aina ikiwemo Mihogo,Chips mayai na wengine walikutwa na Camera ya Blogu ya jamii wakiwa wemebeba vyakula vyao na kujibweda kando kando ya ufukwe,ama kwa hakika ilikuwa burudani kwa wakazi wa jiji la Dar.



Foleni ya kuingia kando kando ya ufukwe nayo ilikuwa kubwa kiasi ambacho magari mengine yalipita kwa taabu kuendelea na safari zake.




Chopa ya Jeshi la polisi nayo ilikuwa na kazi ya ziada kama hivi ya kukagua meneo mbalimbali yaliyokuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu,Pichani chini Chopa ikionekana kwa mbali ilipokuwa ikikatiza maeneo hayo.