Tuesday 24 October 2017

Rekodi za Emmanuel Okwi katika Uwanja wa Uhuru hizi hapa

Zikiwa zimesalia siku chache kuelekea katika mtanange wa watani wa jadi, Yanga SC ambao ndiyo wenyeji wa kiwakaribisha Simba SC katika Uwanja wa Uhuru Octoba 28 mwaka huu mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara.


Hizi ndizo rekodi chache tu za mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda na klabu ya Simba, Emmanuel Okwi katika Uwanja wa Uhuru toka sajiliwe msimu huu.

Emmanuel Okwi ambaye ni kinara wa mabao ndani ya klabu ya Simba na ligi kuu ya Tanzania Bara kwa kufikisha jumla ya magoli 8 katika msimu huu mpya wa 2017/18 amejiwekea rekodi ya kufunga kwenye mechi nne alizoshuka Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.

Mabao nane aliyoyapata Okwi magoli 4 dhidi ya Ruvu Shooting, 2 dhidi ya Mwadui, goli 1 dhidi ya Mtibwa na 1 kwenye ushindi wa 4 -0 dhidi ya Njombe Mji.