Tuesday 24 October 2017

SIMULIZI: SHANIA PART 02 EP 05


..........iilipoishia

Mike alimwambia"Mmmmmh kazi mnao lakini wewe ulikuwa unatakaje"......Pacha wa Shaina alijitengenezea koo vizur"mh!!mh!!! mike jomouny kwanini unakuwa mgumu kunielewa"......Mike alimwambia "Oukey nimeshakuelewa twende kwanza Huko dukani tukirudi tutaongea vizuri.Shania alijipa ushindi mkubwa na kujisemea kimoyo moyo" Yeees!!"kisha
akamwambia"Sawa mike naomba unisaidie jomouun"........"Ondoa shaka".Waliendelea na kasafari chao mpaka barabarani,Walisubiri muda mfupi tuu wakapata kausafiri/Bajaji.........

Basi shania alijisemea "Awamu hii hamchomoi vibaka nyie mnajifanya wachungaji sijui waumini hapa kwangu hakunaga hizo".Mike alianza kuwaza mengi sana" Nikiweza kumbadili tabia huyu binti nitamuoa kabisa naona kama anaelekea ni mwanamke anayejali"Mike alianza kusahau kuwa huyu sio mtu wa kawaida.Walifika Supermarket na kuchukua mazaga na vinywaji kibao,Mike alimuona shania akichagua vileo/pombe"We shania nini hiyo unachukua??".......Shania alimuuliza"Kwani hii hamtumii?......"Wenzangu wanatumia lakini nisingependa uchukue".......Shania alimfuata kwa ukaribu kabisa kisha akamwambia"Mike sikia nikuambie my hii ni mvinyo tuu wala haina shida,Halafu usiwanyime wenzako raha kisa wewe hutumii sawa acha mi nichukue".

Mike hakutaka kabisa kubeba mipombe lakini ndio hivyo maneno ya mwanamke yamemlegeza kisawasawa.Basi Shania alibeba mipombe mingi kuliko hata chakula,Walinunua vitu vya sh 450000/ kwani walichukua wine zile za bei ghali.Walianza kutoka nje ya supermarket shania akiwa amemshika mike kiunoni huku mike akiwa amebeba mazaga kwenye mifuko.Walifika nje na kumkuta dereva wao akiwa anawasubiri shania alimwambia dereva bajaji"Kaka samahani kwa kukuchelewa lakini utatupigia mahesabu mpaka huu muda tulioutumia hapa.Safar ilianza kuelekea fukweni kule waliko kina Luke.Wakati huo kina Luke walikuwa wakisubir ujio wa Mike na Bibie Shania.Dean alianza kupata hisia tofauti"Oyaa mbona jamaa wamechelewa hivi??".......Luke alidakia"Dean unajua ni nini,Huu mtaa huku hakuna supermarket ithink wameenda mbali kidogo".Basi waliendelea kukaanga visamaki vyao,Wakati huo kajua nacho kalikuwa kanaelekea kutuama.Mara wakasikia kimlio cha bajaji na wote walisimama.

Kina Lois walianza kushangilia"Oooooyoooo!!!"Kibajaji kikafika na kupark.Alishuka shania,Halafu akafuata Mike akiwa amebebelea vifuko vya supermarket.Basi Shania alimuuliza dereva bajaji "Shilingi ngapi kaka"......" ni shilingi 20000/dada yangu".Shania alichomoa mkwanja mrefu kisha akamuhesabia elfu 30 kisha akamwambia"Hiyo nyingine ni ya usumbufu".....Mshkaji wa bajaji alishukuru sana kisha akasepa zake.Waliweka ile mifuko pale nje na kuanza kuanza kutoa vitu watakavyotumia jioni ya leo.Basi mapocho pocho yaliandaliwa watu wakala mpaka wakasaza,Shania alimpa Dean ule mfuko wenye chupa za pombe kisha akamwambia hii weka ndani kesho ni wikiendi kwa hiyo tutatumia hii kesho.Dean alichungulia ndani ya mfuko kisha akawaambia wenzake "Oyaaa kesho ni full happy"........ Luke akadakia"Kwani kesho si tunasepa tukinukishe leo bhana aaaah!!"...... Shania akadakia"Hamuwezi kuondoka keaho wakati kesho ni Ijumaa wikiendi hapa kuondoka ni Jumapili"...... Wote walicheka kwa furaha kwani itakuwa ni bata juu ya bata.

Chakula kilishaandaliwa na Luke akapendekeza"Basi tunyweni hata chupa moja ya wine kuondoa strees"....... Shania akamwambia "haya nenda kalete maana una uchu sana wewe". Luke alishusha wine pale na kujimiminia ya kutosha,Wakati huo mike amekaa anakula huku akiwaza kile alichoambiwa na Shania"Hivi nimkubalie huyu dada au niachane naye,Mungu wangu haya ni majaribu gani tena!!?Lakini mbona anaonekana hana shida kabisa anyway itakavyokuwa".Mike na uchungaji wake leo kashindwa kabisa kujicotrol.Walimaliza kula wakaanza kupiga story mpaka saa tano za usiku,Shania aliwaambia" Jamani mimi mwenzenu nshaanza kusikia usingizi".....Wote walisema basi tukalaleni tuu.Nyumba hiyo ilikuwa na vigodoro vya kulalia Vitatu tuu,Walimpa shania kimoja ili alale mwenyewe kisha wao wakajibana kwenye vigodoro viwili.Lakini kabla hawajalala Shania alimuita Mike na kumnong'oneza"Sasa!!badae wakilala wenzako njoo basi tulale wote......Mike aligugumia sauti"mmmmmh!!! yamekuwa hayo!!!? anyway ntaangalia".......Usikose kigongo kinachofuata