Tuesday 26 September 2017

Joti atoa shavu kwa vijana

Kama unakipaji kwa nini ufe na njaa, haya ni baadhi ya maneno yanayopatikana katika ngoma ya ‘Mtazamo’ iliyofanywa na Profesa Jay, Afande Sele na Solo Thang.


Kudhihirisha maneno hayo mchekeshaji nguli Tanzania, kutoka Orijino Komedi Joti ambaye kwa sasa anafanya kazi zake binafsi za uchekeshaji ametoa shavu kwa vijana waliyo na kipaji cha kufanya sanaa ya uchekeshaji ambayo anafanya.

Joti amekuwa akiachia mfululizo wa video za kuchekesha katika mtandao wa YouTube ametoa nafasi hiyo kwa vijana wanaochipukia katika fani ya uchekeshaji kwa kuwataka warekodi video fupi isiyozidi dakika moja iliwaonyeshe uwezo wao kisha atakayekuwa amefanya vizuri na anavutiwa naye basi watafanya kazi pamoja kwa siku zijazo.